Busanda-Geita
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe Martine Shigela, Aprili 12,2025 amefanyaziara katika kata ya Bukoli na Nyarugusu jimbo la Busanda Halmashauri ya Wilayaya Geita.
Katika Ziara hiyo Mhe Shigela amekagua maendeleo ya Ujenzi wa Kituo cha Afya Bukoli kinachojengwa kwa mapato ya ndani ya Halmashauri chenyethamani ya Shilingi Milioni 400.
Pamoja na Kutembelea Zahanati hiyo Mhe.Shigela ametembela pia mradi wa Bweni la Wasichana lenye uwezo wa kubeba wanafunzi 80 katika shule yaSekondari Evaristi iliyopo Kata ya Nyarugusu mradi unaotekelezwa kupitiamfuko wa maendeleo kwa jamii (TASAF) kwa kushirikiana na wananchi kwa gharamaya Shilingi Milioni 180.7 ambapo asilimia 20 ya mradi ni nguvu za wananchi.
Akikagua miradi hiyo Mhe Mkuu wa Mkoa ameonyesha kufarijika kwanamna ambavyo Halmashauri inatekeleza miradi hiyo.
" Safari ya Maendeleo ni safari isiyosimama, Serikaliitaendelea kuboresha huduma katika vituo vya afya ikiwa ni pamoja na kuboreshamiundombinu ya barabara, tuendelee kumpa ushirikiano Mhe Dkt Samia Suluhu HassanRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa namna ambavyo analetaMaendeleo" Amesema Mhe Shigela.
Maendeleo ya Ujenzi wa Kituo cha Afya Bukoli kinachojengwa kwa mapato ya ndani ya Halmashauri chenye thamani ya Shilingi Milioni 400.
Mradi wa Bweni la Wasichana lenye uwezo wa kubeba wanafunzi 80 katika shule ya Sekondari Evaristi iliyopo Kata ya Nyarugusu mradi unaotekelezwa kupitia mfuko wa maendeleo kwa jamii (TASAF) kwa kushirikiana na wananchi kwa gharamaya Shilingi Milioni 180.7
Pamoja na hayo Mhe Shigela amesikiliza kero mbalimbali za wananchizikiwepo kero za miundombinu ya barabara, elimu, maji, umeme, wanufaikawa fedha za TASAF na kuzitolea majawabu ambapo amewaagiza wakuu wa Taasisimbalimbali alizoambatana nazo kushughulikia changamoto za wananchi.
Wananchi wakitoa Kero kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe Martin Shigela wakati alipofanya Mkutano wa Hadhara kusikiliza kero mbalimbali za Wananchi
Katika Ziara hiyo Mhe Mkuu wa Mkoa aliambatana na viongozimbalimbali wakiwepo Mkuu wa Wilaya ya Geita, Mkurugenzi Mtendaji , KatibuTawala wilaya na Wakuu wa Idara na Vitengo kutoka Taasisi, Halmashauri yaWilaya ya Geita pamoja na Kamati za ulinzi na usalama
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa