Timu ya wataalam Halmashauri ya wilaya ya Geita ikiongozwa na Afisa Mipango (W) Bi Sarah Yohana Novemba 2, 2024 imefanya ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi inayo tekelezwa kupitia wajibu wa kampuni kwa jamii (CSR) kutoka mgodi wa dhahabu wa Geita (GGML)
Ziara hiyo imekuwa na lengo la kujua changamoto zinazopelekea kuchelewa kukamilika kwa miradi hiyo ili ianze kutoa huduma kwa wananchi
Mradi wa Kituo cha Afya Kakubilo wenye jengo la mama na mtoto, OPD, Maabara na nyumba ya mtumishi.Mradi huu ni mpango wa CSR mwaka 2021 upo hatua ya mwisho ya ukamilishaji na kwa sasa wananchi wanaendelea kupata huduma katika zahanati hiyo.
Wakiwa katika ziara hiyo, timu imebaini kutokuwepo kwa mafundi ujenzi kwenye miradi huku nyingine ikiwa ni ucheleweshaji wa malipo na vifaa katika baadhi ya miradi.
Mradi wa Zahanati ya Nyawilimilwa ambayo ujenzi wake unaendelezwa ili kuifanya Zahanati hiyo kuwa Kituo cha Afya.Timu imemtaka fundi anayetekeleza mradi huo kuhakikisha anakuwa kwenye mradi (Site) ili kuendelea na kazi zilizobakia kwani wananchi wanasubiri mradi huo ukamilike ili uanze kutumika.
Pamoja na hayo timu hiyo imetoa maelekezo kwa mafundi kuhakikisha wanakuwa kwenye Miradi (Site) kwa ajili ya ukamilishaji wa kazi zilibakia ili majengo hayo yakamilike yaweze kutumika kutoa huduma kwa wananchi
Mradi wa Shule ya Msingi Kata ya Nyawilimilwa wenye thamani ya milioni 300. Shule hiyo yenye madarasa 5, matundu ya vyoo 12 ya wanafunzi na matundu ya vyoo manne kwa ajili ya walimu ujenzi wake umekamilika na inatarajiwa kuanza kutumika ifikapo Januari 2025. Huu ni mradi wa CRS mwaka 2022.
Aidha timu imetembelea mradi wa ujenzi wa soko la Samaki kata ya Nkome ambalo bado utekelezaji wake haujaanza huku hatua za michoro za soko hilo zikiwa zimekamilika. Ujenzi wa soko la Samaki nkome lenye thamani ya milioni 500 utakapokamilika utaweza kuhudumia zaidi yab wananchi elfu 50 kutoka visiwa vya Izumacheli, Butwa na Lulegeya.
Pia timu hiyo imetembelea Zahanati ya Nkome iliyopo kata ya Nkome ambapo Mradi huo unatarajiwa kutoa huduma kwa wananchi zaidi ya eflu 50.
Ukamilishaji wa Zahanati ya Nkome yenye majengo ya OPD, Maabara, Jengo la mama na mtoto. Serikali kuu imetoa kiasi cha shilingi milioni 426 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la upasuaji ( Theatre na Laundry room). Zahanati ya Nkome inatarajiwa kuhudumia zaidi ya wananchi elfu 50.
Serikali kuu inayo ongonzwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuhakikisha Wananchi wanapata huduma bora imetoa fedha kiasi cha shilingi 426 milioni kwa ajili ya ujenzi wa jengo la upasuaji (Theatre na Laundry room).
Vilevile timu hiyo imetembelea Mradi wa ukarabati wa mwalo wa Nkome Mchangani wenye thamani ya kiasi cha shilingi milioni 85 na ujenzi wa vizimba (fish cage) vya Samaki wenye thamani ya Shilingi million 220
Uchumi wa wananchi waliowengi wa kata ya Nkome hutegemea uvuvi wa samaki. Kwa kulitambua hilo Serikali kupitia mfuko wa CSR imeanza mpango wa ukarabati wa mwalo wa Nkome Mchangani kwa kiasi cha shilingi milioni 85 na ujenzi wa Vizimba (Fish cage) wenye thamani ya shilingi milioni 220.
Katika kuhakikisha wanafunzi wanajifunza masomo ya Sayansi kwa vitendo, timu iliweka kutembelea Ukamalishaji wa maabara Shule ya Sekondari ambayo ujenzi wake bado unaendelea huku vyumba vingine vikiwa vimekamilika na Wanafunzi kuendelea kujifunza.
Mwalimu Efraim Kyombo ni mwalimu wa masomo ya Kemia na Bailogia Shule ya Sekondari Nkome ambapo amesema maabara hizo zina vifaa na zimeanza kutumika na wanafunzi wanajifunza kwa vitendo ikiwepo kufanyika kwa mitihani ya Taifa.
Ukamilishaji wa maabara ya Shule ya Sekondari Nkome. Jengo moja la maabara hizo limekamilika ambapo wanafunzi wanaendelea kujifunza kwa vitendo masomo ya Sayansi.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita itaendelea kushirikiana na kufuatilia Miradi ya Maendeleo inayo tekelezwa kupitia wajibu wa kampuni za madini katika jamii (CSR) ili kuhakikisha Miradi hiyo inakamilika na kuanza kuto huduma kwa Wananchi ili waendelee kuwa na imani na Serikali yao.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa