Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Geita Ndg Karia Rajab Magaro, Julai 15, 2024 ameongoza timu ya menejimenti (CMT) kutembelea na kukagua vyanzo vya mapato mamlaka ya mji mdogo Katoro.
Timu hiyo imetembelea vibanda vya biashara, machinjio ya mifugo na Mnada kata ya Katoro kukagua shughuli zinazofanyika maeneo hayo ili kuona namna ya uboreshaji wa miundombinu katika vyanzo hivyo ili kudhibiti upotevu wa mapato.
Timu ya Menejimenti ikiwa kwenye Mnada wa Ng’ombe uliopo Kata ya Katoro. Mnada huo kwa siku za mnada takribani ng’ombe 2000 wanaingia kwenye mnada huo.
Timu ya Menejimenti ikiwa kwenye Kiwanda cha kukunja mabati kilichopo mamlaka ya mji mdogo wa Katoro ambapo timu hiyo imepokea maelezo namna ambavyo kiwanda hicho kinafanya kazi.
Aidha Mkurugenzi ameagiza wasimamizi wa vyanzo hivyo kuhakikisha mazingira yanatunzwa pamoja na kuzingatia swala zima la usafi ili Halmashauri iendelee kukusanya mapato katika vyanzo hivyo vya machinjio na mnada.
Timu ya Menejimeti ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Geita ikiwa kwenye Machinjio ya mifugo kata ya Katoro ambapo kwa siku takribani ng’ombe 10-15 wanachinjwa huku mbuzi wakiwa takribani 10-20. Magaro ameelekeza miundombinu ya Machinjio hayo kuboreshwa na kuwa katika hali ya usafi
Pamoja na kutembelea vyanzo hivyo, pia timu hiyo ilitembelea daraja linalojengwa na TARURA kupitia kampuni ya Treasure Ltd ya Mwanza kwa gharama za Shilingi Milioni 81. Daraja hilo linaunganisha barabara ya CCM-Mtunduni-Mnadani na unatarajiwa kukamilika Agosti 1, 2024 ambapo utarahisisha usafirishaji wa mifugo kuelekea mnadani.
Timu ya Menejimenti (CMT) ikikagua maendeleo ya ujenzi wa daraja linalounganisha barabara ya CCM-Mtunduni-Mnadani wenye thamani ya shilingi Milioni 81.Daraja hilo litarahisisha usafirishaji wa mifugo kuelekea mnada wa katoro wenye uwezo wa kubeba takribani ng’ombe 2000.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa