Wakala wa Barabara za Mji na Vijijini (TARURA) Kwa mwaka wa fedha 2022/2023 imepanga kufanya matengenezo ya barabara na madaraja kwa Kiasi cha shilingi 7,118,678,127 kutoka fedha za mfuko wa Barabara (Road Fund), fedha za tozo na fedha za majimbo ya Geita vijijini, Geita Mji na Busanda.
Taarifa iliyowasilishwa katika kikao cha baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Februari 3, 2022 na Kaimu Meneja wa TARURA Wilaya ya Geita Mhandisi Thereza Bernado imeeleza kuwa matengenezo hayo yamegawanyika katika sehemu nne ambazo ni matengenezo ya kawaida, matengenezo ya muda maalumu, matengenezo ya sehemu korofi na madaraja.
Kwa Halmashauri ya Wilaya ya Geita mapendekezo ya TARURA kwa matengenezo ya kawaida kwa mwaka wa fedha 2022/2023 yanatarajiwa kugharimu jumla ya kiasi cha Tshs.260,000,000 (milioni 260) kwa kata za Nyamalimbe, Kamena, Busanda, Lwamgasa/Nyarugusu na Nyawilimilwa.
Kwa upande wa mapendekezo ya matengenezo ya sehemu korofi katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita TARURA imepanga kutumia jumla ya kiasi cha Tshs. 858,000,000 (milioni 858) kwa kata za Nkome, Kasota, Nyawilimilwa, Nyaruyeye, Lwamgasa/Nyarugusu, Katoro, Nyakagomba, Nyamwilolelwa, Lubanga, Busanda, Kamena na Nyamalimbe.
Aidha kwa Mapendekezo ya matengenezo ya muda maalumu Halmashauri ya Wilaya ya Geita imetengewa jumla ya kiasi cha Tshs. 440,000,000 (milioni 440) kwa kata za Kamena, Lubanga, Nyamwilolelwa, Nyakagomba, Lwamgasa/Nyarugusu, Nyawilimilwa, na Nkome.
Kwa upande wa ujenzi wa madaraja Halmashauri ya Wilaya ya Geita imetengewa jumla ya kiasi cha Tshs. 270,000,000 (milioni 270) katika kata za Katoro, Nkome, Kasota, Nyawilimilwa, Nyaruyeye, Lwamgasa/Nyarugusu, Nyakagomba, Nyamwilolelwa, Lubanga, Busanda, Kamena na Nyamalimbe.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita inahudumia mtandao wa barabara za vijijini (Collector, Feeder and Community Roads) wenye jumla ya Kilometa 1745 ambapo kati ya hizo barabara za Changarawe ni Kilometa 600.8, barabara za udongo ni kilometa 1144.99 na jumla ya madaraja 460.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa