Wananchi Mkoani Geita wamepongeza kasi ya Ujenzi wa mradi wa soko kubwa la kisasa linalojengwa Katoro ndani ya Halmashauri ya Wilaya Geita linalotazamiwa kumaliza Desemba 2020
Mhandisi wa mradi huo kutoka Suma JKT Mhandisi Shimwesa Saidi amesema kasi ya ujenzi wa soko hilo inachagizwa na upatikanaji wa vifaa kwa haraka na ushirikiano kutoka halmashauri wilaya ya Geita pamojana na fedha za uwajibikaji kwa jamii
Wananchi wa Katoro wamepongea hatua ya ujenzi huku wakiamini itaongeza chachu ya maendeleo kwa jamii na kukua kwa muingiliano wa kibiashara Afrika Mashariki na Kati
Wakati huohuo mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilaya ya Geita Barnabas Mapande amesema utekelezaji wa mradi huo mkubwa ni alama ya kukua kwa maendeleo ndani ya mkoa wa Geita.
Mradi huo wa soko kubwa la kisasa mji mdogo wa katoro unatajwa kugharimu zaidi ya shilingi bilioni 2 na soko hilo litakuwa katika orodha ya masoko bora zaidi ukanda wa Afrika Mashariki na kati.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa