Afisa elimu mkoa wa Geita Yesse Kanyuma amewasisitiza wakuu wa shule za msingi pamoja na sekondari kuanzisha na kutumia ipasavyo kamati za udhibiti ubora ndani ya shule ili kuboresha elimu na kuwezesha shule kuendeshwa kwa kufuata misingi, sheria na taratibu za elimu nchini.
Hayo ameyaeleza alipokuwa kwenye ziara ya kufuatilia ujenzi wa maboma ; mikakati ya ufundishaji na ujifunzaji kwa madarasa ya mitihani; kusoma, kuandika na kuhesabu( KKK); utawala na uendeshaji wa shule katika shule za kata zilizopo ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Geita na mkoa kwa ujumla.
Akizungumza na wakuu wa shule, maafisa elimu kata, wenyeviti na wajumbe wa kamati za bodi za shule pamoja na walimu shule za msingi na sekondari za Kagu, Bugulula na Bugando, Kanyuma amesema kuwa wadhibiti ubora wakifanya kazi zao vizuri na kutumiwa ipasavyo katika kufanya tathimini mbalimbali , itasaidia katika maendeleo ya elimu shuleni.
Katika ziara hiyo aliambatana na maafisa elimu taaluma kutoka idara ya elimu mkoa, baadhi ya watumishi wa idara za elimu msingi na sekondari Halmashauri ya wilaya Geita wakiwemo wakuu wa idara hizo amezitaka idara zote za shule kuwa na mpango mkakati wa ufundishaji, kumaliza mada kwa wakati,
Mkuu huyo amesisitiza pia uwepo wa mitihani ya kujipima kwa wanafunzi, kuwa na vikao vya taaluma kujadili masuala ya ufundishaji na changamoto, motisha kwa walimu na wanafunzi wanaofanya vizuri, wanafunzi kuwa na vikao vyao lakini pia amepongeza baadhi ya shule kwa kukamilisha ujenzi wa maboma kabla ya tarehe iliyopangwa.
Mkuu wa idara ya elimu msingi Halmashauri ya Wilaya ya Geita Saidi Matiko amesema wameweka taratibu mbalimbali za kudhibiti utoro wa walimu pia amewataka walimu kuweka maazimio kila wanapokutana kwenye vikao vyao ili kurahisisha utekelezaji wa shughuli za shule.
Kwa upande wake afisa elimu Sekondari Richard Mwakihaba amewataka walimu kuwajibika ipasavyo katika ufundishaji wanafunzi ili kuboresha ufaulu pamoja na kuendana na kasi ya serikali ya awamu ya tano katika uboreshaji elimu pia kutoa elimu bila malipo.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa