Wananchi pamoja na kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi(CCM) wamejitokeza kuchimba msingi wa ujenzi wa shule ya sekondari yenye ghorofa inayojengwa katika kijiji cha Kasota, kata ya Bugulula ndani ya Halmashauri ya wilaya ya Geita.
Akizungumza katika zoezi hilo, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Geita Barnabas Mapande amesema kuwa zaidi ya madarasa 36 yatajengwa katika shule hiyo ambayo yatasaidia wanafunzi wanaohitimu kwenye shule mbalimbali za msingi katika maeneo hayo.
Nae Afisa Elimu Sekondari wa halmashauri ya wilaya Geita, Richard Mwakihaba amesema majengo ya shule hiyo yatajengwa kwa awamu na yatagharimu kiasi cha shilingi bilioni 4.2.
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Geita Ali Kidwaka amesema sababu yakuamua kujenga shule hiyo ni kutokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya wanafunzi katika kijiji hicho cha Kasota.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa