Serikali imesema kuwa, itaenda kushughulikia changamoto kwenye sekta za Afya, Elimu, pamoja na miundombinu ya Barabara ambazo zimekua zikiikumba Kata ya Lwamgasa.
Hayo yamebainishwa na Naibu Wazir kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI, anayeshughulikia masuala ya Afya, Mhe. Dkt Jafari Rajabu (Mb), Disemba 20 katika Kata ya Lwamgasa wakati akihitimisha ziara yake ya kikazi ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Geita.
Akizungumza na wananchi wa Kata hiyo wakati akitolea ufafanuzi changamoto hizo zilizoibuliwa na Diwani wa Kata hiyo Mhe. Dkt. Daniel Mabala, Dkt. Jafari amesema kuwa serikali imejipanga kuhakiksha kuwa inaleta ahueni kwa wananchi kwa kuwapatia unafuu kwenye huduma zote za msingi.
"Kuanzia mwakani, kama Serikali tuna mpango wa kuongeza idadi ya watumishi katika sekta ya afya kwenye zahanati zetu na vituo vya afya, haswa vijijin ili wananchi waweze kupata huduma kwa urahisi. Pia tutahakikisha dawa zinapatikana pamoja na kuwepo gari la wagonjwa pindi Kituo chetu kipya cha afya kitakapoanza kazi." Amesema Dkt. Jafari.
Dkt. Jafari ameongeza kwa kusema kuwa tayari serikali imetenga fedha ili kuyamalizia maboma kwenye shule za Msingi na Sekondari ili wanafunzi waweze kuanza kusoma mnamo Januari mwakani.
Aidha, ameiagiza wakala wa barabara, TANROADS kuhakiksha inakamilisha barabara zinazoiunganisha Lwamgasa pamoja na Kata za Katoro na Nyarugusu kwa kiwango cha Lami ili kurahisisha shughuli za kiuchumi haswa kipindi cha mvua.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa