Nanenane-Mwanza
Maenesho ya Nanenane Kanda ya Ziwa Magharibi 2025 yamehitimishwa leo Agosti 08,2025 katika Viwanja vya Nyamhongolo Jijini Mwanza.
Akizungumza katika Kilele cha Sherehe za Nanenane Mgeni Rasmi Mhe Said Mtanda ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza amewapongeza Waandaji wa Maonesho hayo Mkoa wa Geita na Mwanza ambapo amewataka Kuyafanya Kuwa bora zaidi kwa Mwakani.
Aidha Mhe Mtanda amewataka Wakulima na Wananchi kuyatumia Maonesho hayo kuendelea Kujifunza ili kuboresha kazi zao ili kuweza kuleta Maisha bora kwa kila mmoja.
Pamoja na Hayo Mhe Mtanda ameishukuru Serikali ya awamu ya Sita inayo ongozwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuleta fedha kwa ajili ya Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi. " Kwa mwaka 2020-2025 Serikali imetoa mbolea ya Ruzuku yenye thamani ya shilingi Bilioni 6.4 sawa na Tani 9192" Amesema Mhe Mtanda.
Vilevile Mkuu huyo wa Mkoa wa Mwanza amesema jumla ya Shilingi Bilioni 4.7 zimetolewa na Serikali kwa ajili ya ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba kwa Mkoa wa Geita na Mwanza ambapo jumla ya vikundi 42 vyenye vizimba 201 vimefaidika na mradi huo.
Akizungumza kuhusu Sekta ya Kilimo cha Umwagiliaji, Mhe Mtanda amesema Serikali imetoa Bilioni 40.2 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa miradi 9 ya umwagiliaji ambapo miradi 34 inaendelea kufanyiwa upembuzi yakinifu ili kuongeza wigo wa miradi ya umwagiliaji katika Mkoa wa Geita na Mwanza.
" Miradi hii itakapokamilika itawanufaisha wananchi na wakulima takribani elfu 40." Ameongeza Mhe Mtanda.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita ni Miongoni mwa Washiriki katika Maonesho hayo ambapo Imepata Cheti cha Pongezi na Kikombe kama Mshindi wa Tatu kwa Halmashauri za Mkoa wa Geita na Mwanza.
Maonesho hayo yamebebwa na Kauli mbiu isemayo" Chagua Viongozi Bora Kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi 2025"
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa