• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Halmashauri ya Wilaya ya Geita

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
        • TASAF
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Maji
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Afya
      • Elimu Msingi
        • Utamaduni
      • Elimu Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Manunuzi na Ugavi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • UKIMWI
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Madini
    • Viwanda
    • Biashara
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Uvuvi
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe.Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Elimu,Afya na Maji
      • UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Wahe.Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Sheria ndogo
    • Mpango mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi/kitaifa
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha

SERIKALI YA DKT SAMIA KUFUNGA UMEME JUA KISIWA CHA IZUMACHELI-GEITA DC

Posted on: January 23rd, 2025

Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe Hashim Komba, Januari 21, 2025 amefanya ziara katika Kisiwa cha Izumacheli kilichopo ziwa Viktoria Mkoani Geita.

Mhe Komba katika Ziara hiyo, amekagua mradi wa nyumba ya mtumishi zahanati ya Izumacheli pamoja na Mabweni mawili ya shule ya Sekondari Izumacheli ambapo amefanya uzinduzi wa Mabweni hayo.

Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe Hashim Komba akizungumza na Wanachi wa Kata ya Izumacheli alipofanya Ziara ya kukagua Miradi ya Maendeleo Katika Kata hiyo iliyopo Kisiwani.

Akisoma taarifa  ya ujenzi wa Mabweni ya Wasichana na Wavulana katika shule ya Sekondari Izumacheli, Kaimu Afisa Mtendaji Kata ya Izumacheli Ndg Boniphace Jeremia amesema mradi huo unafadhiliwa na  mfuko wa maendeleo wa jamii(TASAF) ambapo jumla ya Kaya 167  zinanufaika toka mwaka 2020 na kiasi cha Shilingi 194,187,000 zimekwisha pokelewa ikiwa ni ruzuku za walengwa wa mpango kuanzia Julai , 2020 hadi Desemba , 2024.

Mradi wa Mabweni Mawili ya Wavulana na Wasichana yenye uwezo wa kubeba wanafunzi 48 kila moja. Mradi huo Umetekelezwa na Mfuko wa maendeleo ya Jamii (TASAF) kwa kushirikiana na Wanachi  wa Kata ya Izumacheli kwa gharama ya Tsh 203, 291,294.79. Ujenzi wa Mabweni hayo ni jitihada za Serikali kuboresha  miundombinu ya elimu katika shule ya Sekondari Izumacheli 

“Ujenzi wa  Mabweni mawili yenye uwezo wa kubeba wanafunzi 48 kila moja ulianza mwaka 2022/23 kupitia mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF) kwa kushirikiana na wananchi wa kata ya Izumacheli kwa gharama ya Shilingi 203,291,294.79 ambapo asilimia 10 ya gharama za mradi imechangiwa na  wananchi” amesema Kaimu Mtendaji huyo katika taarifa ya mradi huo mbele ya Mhe Komba.

Akizungumza na Wananchi wa Kata ya Izumacheli wakati wa uzinduzi wa Mabweni ya shule ya Sekondari Izumacheli, Mhe Komba amewataka wazazi walezi kuendelea kushikamana na walimu ambao wanafundisha katika Kisiwa hicho  “Niwaombe wana Izumacheli muendelee kuwapenda walimu na kuwapa ushirikiano kwani wanafanya kazi kubwa ya kuwainua kitaaluma watoto wetu” Amesema Mhe Komba.

Mradi wa Nyumba ya Mtumishi wenye thamani ya Shilingi Milioni 102 kutoka mfuko wa pamoja wa Afya. Nyumba hiyo inaenda kuwasaidia watumishi wa Zahanati ya Izumacheli kuishi karibu na Zahanati hiyo kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi

Vilevile amewataka wanafunzi wa shule hiyo kuendelea kujiamini ili kufikia ndoto zao kwa kuepuka vitisho mbalimbali wanavyokutana navyo katika safari ya masomo.

Pamoja na hayo Mhe Komba amewataka wananchi kisiwani humo kudumisha amani na utulivu. “Lazima Mlinde amani na utulivu kwa wivu mkubwa na kama kuna mtu mnaona mienendo yake sio mizuri mtoe taarifa ili vyombo vya ulinzi na usalama viweze kuchukua hatua” Amesisitiza Mhe Komba

Wananchi wa Kata ya Izumacheli wakifuatilia Mkutano wa Hadhara wa Mkuu wa Wilaya wakati wa Uzinduzi wa Mabweni ya Shule ya Sekondari ya Izumacheli

Aidha Mhe Komba ametoa rai kwa wananchi wa Kisiwa hicho  kujiepusha na mambo ambayo yanaweza sababisha  migogoro na kisiwa cha Hifadhi ya  Rubondo ili kuendelea kulinda ustawi wa wananchi.

Hali kadhalika Mhe Komba ameitaka Halmashauri kuhakikisha Kata hiyo inapata Mtendaji wa Kijiji kufuatia mtendaji aliyekuwa akitumika katika kijiji hicho kuwa tatizo na kupelekea kuwa na malalamiko kwa wananchi na migogoro ya madai na malumbano “Niendelee kuwataka watumishi wa umma na wananchi kuwa na umoja na mshikamano ili kusukuma gurudumu la maendeleo.” Ameongeza Mhe Komba.

Pamoja na hayo Mhe Komba amewataka wananchi kuendelea kuwa na imani na Serikali ya awamu ya sita inayo ongozwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan  kwa kuwa Serikali ipo kwenye mchakato wa kufunga umeme Jua katika Kisiwa hicho ili wananchi wanufaike na kuchochea shughuli za maendeleo.

“Dkt Samia Suluhu Hakuna alichokisahau, tumebaki na vijiji 3 kati ya vijiji 158 vya wilaya ya Geita ambavyo havina umeme, Serikali kupitia Wizara ya Nishati inayo ongozwa na Mhe Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dotto Mashaka Biteko (MB) inafanya kazi kubwa kumpa kazi mtu wa Rea kutafuta mzabuni wa kufunga umeme wa jua utakaosambazwa katika vijiji vitatu ili kukamilisha vijiji vyote vya wilaya ya Geita kuwa na umeme.

Katika Ziara hiyo Mhe Mkuu wa Wilaya aliambatana na Katibu Tawala wilaya Bi Lucy Beda, Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Geita pamoja na Wataalam kutoka halimashauri ya Wilaya ya Geita wakiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Bi Sarah Yohana.

Katibu Tawala Wilaya ya Geita Bi Lucy Beda akizungumza na Wananchi wa Kata ya Izumacheli wakati wa Ziara ya ukaguzi wa Miradi ya Afya na Elimu inayotekelezwa katika Kisiwa Hicho

Kisiwa cha Izumacheli ni moja ya Visiwa vitatu ndani ya Izumacheli vyenye makazi ya watu na Serikali ya awamu ya Sita imeendelea kupekeleka huduma za kijamii zikiwepo shule na zahanati. Visiwa vingine vikiwa ni Butwa, Lulegeya na Kisiwa cha Hifadhi ya Rubondo.


Tangazo

  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO KWA VIKUNDI January 23, 2025
  • TANGAZO LA KAZI GEITA DC September 10, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA September 16, 2024
  • Geita Mamlaka za Wilaya na malmaka za miji GP DOM.pdf September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • DC KOMBA ARIDHISHWA NA UTEKEKEZAJI WA MIRADI KUELEKEA MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2025.

    May 06, 2025
  • MEI MOSI YALETA FARAJA KWA MAAFISA TARAFA GEITA.

    May 02, 2025
  • RC SHIGELA AIBUA MATUMAINI MAPYA KWA WATUMISHI MKOANI GEITA.

    May 02, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI GEITA DC LAMPONGEZA MKURUGENZI MTENDAJI KWA KUPATA HATI SAFI

    April 30, 2025
  • Tazama zote

video

DED. WANGA AWATAKIA MTIHANI MWEMA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA WANAOJIANDAA KUFANYA MITIHANI YA TAIFA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Asili ya jina Geita
  • Fursa ya viwanda
  • Fursa ya madini
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA KATI, 2021
  • Vivutio vya Utalii
  • Miradi itakayotekelezwa
  • Miradi inayoendelea
  • Orodha ya wahe.Madiwani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Bofya Hapa Kutuma,Kupokea na Kufuatilia Malalamiko,Mapendekezo,Maulizo na Pongezi Halmashauri ya Wilya ya Geita
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Watumishi Portal
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS)
  • Ofisi ya Rais TAMISEMI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter Widgets

Ramani ya Sehemu

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Geita

    Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita

    Simu: +225 282520061

    Mobile:

    Barua pepe: info@geitadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali na Majibu yanayoulizwa mara kwa mara
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa