Naibu Wazir kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI, anayeshughulikia masuala ya Afya, Mhe. Dkt Jafari Rajabu, ametembelea na kukagua ujenzi wa mradi wa Kituo cha Afya kilichopo Kata ya Lwamgasa, na kuipongeza kampuni ya uchimbaji ya Mgodi wa BUCREEF kwa kuchangia maendeleo kwenye jamii kupitia mpango wa CSR.
Mradi huo unaogharimu kiasi cha Shilingi Milioni 459 ikiwa ni fedha kutoka Serikali Kuu, na Milioni 300 kutoka Mgodi wa Bacreef, unatarajiwa kukamilika mnamo mwezi Febuari, 2026 na kuwa mkombozi kwa wananchi wa Kata hiyo.
Akizungumza wakati wa ziara yake kwenye Kata hiyo, Disemba 20, Mhe. Dkt Jafari ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa mradi huo pamoja na kutoa Pongezi kwa Halmashauri kupitia kwa Mkurugenzi wake kwa kuendelea kusimamia miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali kwenye Halmashauri hiyo.
"Niwapongeze Halmashauri ya Wilaya ya Geita kwa kusimamia miradi hii. Kama jamii tunapaswa kutambua umuhimu wa miradi hii na hivyo ni wajibu wetu kuilinda." Amesema Dkt. Jafari.
Dkt. Jafari pia amemuagiza Mkurugenzi kuhakiksha anashugulikia huduma muhimu za Maji na Umeme ili ziweze kufika kwenye kituo hicho kabla hakijaanza kazi.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa