Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Ndg. Karia Magaro, ametoa wito kwa wanamichezo wanaotarajiwa kujiunga na kambi ya maandalizi kuelekea mashindano ya SHIMISEMITA, Mkoani Tanga, kuwa na nidhamu pamoja na kuongeza juhudi kwenye mazoezi ili waweze kufanya vizuri na kurudi na vikombe.
Akizungumza mwishoni mwa juma lililopita katika viwanja vya shule ya Sekondari ya Wasichana, Nyankumbu alipohudhuria Awamu ya Pili ya Bonanza la Watumishi lililoandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Geita, Ndg. Karia amewasisitiza wanamichezo hao kujifanyia tathmini wawapo mazoezini, ili waweze kutambua madhaifu yao mapema na kuyafanyia kazi kabla ya kuanza kwa mashindano hayo.
Ndg. Karia ametoa angalizo kwa wanamichezo hao kutambua kuwa mashindano ya safari hii yatakua magumu, hivyo wanapaswa kufanya maandalizi ya kujitosheleza ili wanamichezo hao wakatoe ushindani, badala ya kwenda kama washiriki.
Kwa upande wa motisha kwa wachezaji hao, Ndg. Karia amesema kuwa ofisi yake kupitia Kitengo cha Utamaduni, Sanaa na Michezo, itahakikisha inaandaa mazingira rafiki pamoja na kuwawezesha wanamichezo hao wawapo kambini, na pindi mashindano hayo yatakapoanza.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa