Kituo cha Redio Rubondo fm kinachomilikiwa na Halmashauri ya wilaya ya Geita,kimepatiwa hati ya Pongezi kwa kushiriki kikamilifu katika kudhamini tamasha la utalii na maonyesho ya biashara, yaliyofanyika chato mkoani Geita kuanzia agosti 7, 2021 hadi Agosti 15 ,2021.
Mgeni rasmi akiwa Naibu waziri wa maliasili na utalii, Mh.Mary Masanja Agost 15,2021 amefunga rasmi tamasha hilo,ambapo ametoa vyeti kwa taasisi mbalimbali zilizoshiriki kwa hali na mali kudhamini na kufanikisha tamasha hilo, kikiwemo kituo cha redio cha Rubondo fm.
Tamasha hilo la utalii na maonyesho ya biashara wilayani chato limefanyika kwa mara ya kwanza, tangu kutangazwa chato kama kitovu cha utalii kanda ya ziwa mwaka 2019.
Naibu waziri Mh.Mary Masanja amesema serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya hifadhi za kanda ya ziwa Ikiwemo Burigi Chato, ili kuwavutia wawekezaji wengine kwenda kuwekeza,pamoja na watalii kutembelea hifadhi hiyo.
Aidha ameuomba uongozi wa mkoa wa Geita kuhakikisha unawapokea wageni kutoka maeneo mbalimbali wanaokuja Geita kwa kazi zao zingine kama kufanya biashara za dhahabu kuwashawishi kwenda kutembelea hifadhi zilizoko maeneo ya kanda ya ziwa.
Aidha kituo cha Redio cha Rubondo fm kinachosikika katika masafa ya 105.3 mhz mkoani Geita kilichoanzishwa mwaka 2019 , kimekuwa mstari wa mbele katika kushiriki na kuhamasisha kwenye masuala mbalimbali ya kimaendeleo kama inavyosema kauli mbiu ya kituo hicho “RUBONDO FM KWA MAENDELEO YA WATANZANIA”
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa