Naibu waziri wa elimu Sayansi na Tecnolojia William Olenasha ameahidi kupitia Wizara yake kuhakikisha wanatilia mkazo utekelezaji wa haraka wa ujenzi wa chuo cha ufundi VETA, ambao unatakiwa kuendelea katika kata ya Bombambili mkoani Geita.
Olenasha amesema ujenzi wa chuo hicho ulipata changamoto ya mkandarasi ambaye aligundulika amedanganya vielelezo na kujitengenezea uwezo ambao hakua nao, hivyo wakaamua kusitisha mkataba wake.
Aidha Naibu Waziri ameahidi kwenda kuyajadili maombi makuu mawili yaliyowasilishwa na kaimu mkuu wa wilaya ya Geita Thomas Dimme,ambayo ni gari la uthibiti ubora wa shule ili kurahisisha shughuli za ukaguzi pamoja na kuajili baadhi ya watumishi wa idara hiyo, pia ombi la kuajili walimu wa sayansi kwa shule za sekondari na walimu wengine katika idara ya elimu msingi.
Katika hatua nyingine Naibu waziri amepongeza idara ya uthibiti ubora wa shule Halmashauri ya Wilaya ya Geita pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Ali Kidwaka kwa juhudi walizozifanya katika ukamilishaji wa haraka wa jengo la uthibiti ubora ambalo limeshaezekwa,kwasasa lipo katika hatua ya upigaji ripu na uwekaji wa mfumo wa umeme.
Mthibiti mkuu ubora wa shule Wilaya ya Geita Dismas Manyonyi amesema ujenzi wa jengo hilo ulianza tarehe 03/06/2019 na hadi kufikia tarehe 31/07/2019 fundi alikuwa amekamilisha hatua ya kupaua jengo, kazi ya upigaji lipu na dari vilikuwa vinaendelea.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Ali Kidwaka amesema ushirikiano baina yake, wathibiti ubora wa shule pamoja na wataalam mbalimbali wa Halmashauri ndio uliosababisha jengo hilo kukamilika kwa haraka.
Mradi huo wa ujenzi wa ofisi za mthibiti ubora kwa kanda ya ziwa unajumuisha ofisi 15 ambapo mkoa wa Geita umepata ofisi 5, ambazo zinajengwa katika Halmashauri ya Mji na Wilaya Geita, Nyang’wale, Mbogwe pamoja na Chato.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa