Serikali imeendelea kusisitiza kuwa mwisho wa kusajili laini za simu kwa alama za vidole ni desemba 31 mwaka huu.
Msisitizo huo umetolewa na naibu waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Atashasta Nditiye jumatano wakati wa mazungumzo na Rubondo Fm ambapo amesema wale wote watakaoshindwa kusajili laini zao za simu katika muda huo, laini zitazimwa.
Pia naibu waziri Nditiye amesema kuwa Serikali imedhamiria kuweka mfumo wa anuani za makazi na postikodi sehemu mbalimbali nchini ili kuwawezesha wananchi kupata huduma popote pale walipo.
Nae mkuu wa mamlaka ya mawasiliano(TCRA) kanda ya ziwa, Mhandisi Francis Mihayo amesema kuwa zoezi la kusajili laini za simu kwa alama za vidole ni bure na kwamba mwananchi hawapaswi kutozwa fedha yoyote.
Wakati huo huo naibu waziri Nditiye amesema kuwa serikali imetenga shilingi bilioni 65 kwa ajili ya kujenga minara ya mawasiliano kwenye maeneo mbali mbali nchini ili kuwawezesha wananchi kupata huduma za mawasiliano ya simu kwa urahisi
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa