MUSUKUMA AKABIDHI ZAHANATI INAYOTEMBEA
Gari lenye thamani ya zaidi ya milioni 100 limetolewa na mbunge wa Geita vijijini Joseph Kasheku Musukuma ikiwa ni zahanati inayotembea kwenye vijiji mbalimbali vya halmashauri ya wilaya Geita.
Akizungumza wakati wa kukabidhi gari hilo kwa mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Ali Kidwaka, Mbunge Musukuma amesema gari hilo litakuwa na uwezo wa kutoa huduma ya kujifungua kwa wakina mama.
Katika hatua nyingine Mbunge Musukuma ametoa pikipiki 15 kwa makatibu wa chama cha mapinduzi jimbo la Geita vijijini ni katika kutekeleza moja ya ahadi alizoziahidi alipochaguliwa kuwa mbunge.
Kwa upande wake mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Geita Barnabas Mapande amempongeza Mbunge Musukuma kwa maendeleo anayoyaleta na kusema kuwa zahanati hiyo tembezi itakuwa ndio ya kwanza kwa mkoa mzima wa Geita.
Nae mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Geita Ali Kidwaka amesema vitu ambavyo anavileta mbunge Musukuma kwenye Halmashauri yake vinamsaidia kurahisisha utendaji wake.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa