Halmashauri ya Wilaya ya Geita imekamilisha kwa asilimia 100 ujenzi wa mradi wa matundu 23 ya vyoo katika shule ya Msingi Nyamalimbe baada ya kupata fedha kutoka Serikali kuu kupitia mradi wa huduma za maji,elimu ya afya na usafi wa mazingira (School Walter,Sanitation and hygiene) SWASH uliogharimu jumla ya shilingi milioni thelathini na sita, laki nne na elfu thelathini na nane na sabini na mbili na senti kumi na moja (36,438,072.11).
Kukamilika kwa mradi huu sasa kutasaidia kupunguza changamoto ya wanafunzi wa kike wanaofikia umri wa kuvunja ungo na kubaki nyumbani kwa kuhofia mazingira salama ya kujisitiri, kwasababu ujenzi huo umezingatia pia kutenga chumba maalumu (chumba cha hedhi salama) kwa wasichana wanaopatwa na hali hiyo pamoja na kupunguza magonjwa ya milipuko na magonjwa ya kuambukiza kwa wanafunzi na watumishi.
Kuwepo kwa chumba hicho maalumu cha hedhi salama kwa wanafunzi wa kike kunaifanya shule ya msingi Nyamalimbe kuwa ya mfano Katika Wilaya ya Geita kwa kuwa ujenzi wa vyoo katika shule nyingi haujazingatia jambo hilo.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi –CCM Wilaya ya Geita Barnabas Mapande na kamati ya siasa leo Septemba 15, 2021 amefanya ziara katika shule ya msingi Nyamalimbe na kupongeza jitihada za maendeleo zilizofanyika mpaka kukamilika kwa mradi na kuonesha kufurahishwa zaidi na uwepo wa chumba cha hedhi salama kwa wasichana.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa