Timu ya watumishi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Geita imewasili jijini Tanga kushiriki mashindano ya SHIMISEMITA yaliyoanza leo Agosti 15 hadi 29, 2025.
Akizungumza katika ufunguzi wa mashindano hayo, Mwenyekiti wa timu hiyo, Mwl. Raphael Ngeleja, amesema wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri, wakiwa na morali na ari ya kutetea ubingwa wa mpira wa miguu pamoja na vikombe vingine, kutokana na maandalizi mazuri waliyoyapata. Ameongeza kwa kumpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita kwa kuwasaidia kuanzia kipindi cha kambi hadi kufika jijini Tanga.
Kwa upande wake, mchezaji wa mpira wa pete (netball) ambaye pia ni mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Mary Gunda, amesema mashindano haya yanachochea mshikamano na kuhamasisha amani kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao. “Uwepo wetu Tanga ni ishara ya amani. Tunawahimiza wananchi wote kushiriki uchaguzi wa mwaka 2025 kwa amani, upendo na mshikamano,” alisema.
Naye Neema George, mchezaji wa mpira wa pete na mpira wa mikono (handball), ametoa onyo kwa timu pinzani akisema: “Timu kutoka wilaya nyingine zijiandae kukutana na upinzani mkali kutoka Geita DC kwani tumejipanga vyema.”
Mashindano hayo yatafanyika katika viwanja mbalimbali jijini Tanga, ambapo timu ya mpira wa miguu ya Geita DC itaanza kwa kuvaana na Kyerwa DC kwenye Uwanja wa Usagara Sekondari
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa