Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhe. Martin Shigela Septemba 22, 2024 amefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo itakayotembelewa na Mwenge wa Uhuru unaotarajiwa kupokelewa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Octoba 05, 2024.
Katika ziara hiyo Mhe Shigela ameambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Geita sambamba na Mkuu wa Wilaya ya Geita, Mhe. Abdallah Komba, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita, na wataalamu mbalimbali kutoka halmashauri ya Wilaya ya Geita.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Martin Shigela (katikati) akizungumza jambo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Dr Modest Lwakahemula (kulia) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe. Hashim Komba (Kushoto) alipokagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha afya cha Nkome katika kata ya Nkome.
Akiwa katika kata ya Nkome Mhe. Shigela ametembelea mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya cha Nkome, ambako amesifu hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa kituo hicho, akizingatia ubora wa ujenzi na miundombinu ya kisasa katika kituo hicho. Mhe Shigela pia ametoa pongezi kwa Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, na Diwani wa Kata ya Nkome kwa usimamizi mzuri wa fedha za serikali katika ukamilishaji wa mradi huo.
Mwonekano wa kituo cha Afya cha Nkome, kilichopo kata ya Nkome.
Baada ya ziara Nkome, Mhe. Shigela alikagua ujenzi wa ofisi ya Kata ya Nzera, ambao ujenzi wake umekamilika. Mkuu wa Mkoa akiwa katika mradi wa ofisi ya Kata Nzera alitoa ushauri kuhusu maboresho kadhaa yatakayosaidia kuimarisha zaidi mazingira na mwonekano wa ofisi hiyo ili watumishi ambao serikali inaendelea kuajiri waweze kufurahia mazingira mazuri ya ofisi hizo.
Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe. Hashim Komba (wa pili kulia) akieleza hatua zilizofikiwa katika mradi wa ujenzi wa ofisi ya kata ya Nzera kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Martin Shigela (wa kwanza kulia).
Mwonekano wa ofisi ya kata ya Nzera
Mkuu wa Mkoa aliipongeza timu ya usimamizi wa miradi kwa kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati ili iweze kuhudumia wananchi. "Ni muhimu kuhakikisha miradi yote inakamilika ipasavyo na si kuchukua muda mrefu bila kukamilika, jambo ambalo linaweza kuathiri matumizi na huduma kwa wananchi" Amesisitiza Shigela.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa