Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Geita John Paul Wanga ameshauri kuangalia namna ya kutoa hamasa kwa walimu kulingana na mazingira yao ili kuongeza ufanisi wa majukumu yao hali itakayoiwezesha Halmashauri ya wilaya ya Geita kupata matokeo mazuri zaidi katika mitihani ya taifa.
Ameeleza hayo agosti 12,2021 wakati akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani wa wilaya ya Geita kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya hiyo Nzera,wakati akieleza vipaumbele vyake 14 atakavyojielekeza navyo katika utumishi wake akiwa Halmashauri ya wilaya ya Geita.
Amesema kuwa “Geita ya dhahabu haiwezi kuwa ya mwisho”,huku akizitaka serikali kuanzia ngazi za vijiji kuwa na mikakati ya kuboresha miundombinu ya Elimu, hali itakayoleta matokeo mazuri, huku akisisitiza kuwa, ’’Geita kuwa ya kwanza kitaifa inawezekana”.
Amezungumzia utoro kwa wanafunzi kuwa ni changamoto inayorudisha nyuma maendeleo ya elimu,huku akitoa rai kwa viongozi kuanzia ngazi za chini ambao wanaishi na jamii kwa ukaribu kuisaidia serikali katika kudhibiti utoro kwa kuwa wanafunzi watoro wanachangia kuirudisha nyuma halmashauri ya wilaya ya Geita hasa kwa kutokufanya vizuri katika mitihani yao ya taifa.
Aidha ameshauri kuwa kuliko kuendelea kujenga vyumba vya madarasa kwenye shule zenye changamoto ya wingi wa wanafunzi ni vyema kuanzisha shule nyingine mpya maeneo mengine ili pia kuwapunguzia wanafunzi kadhia ya kutembea umbali mrefu kuzifuata shule
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa