Katika kuhakiksha wananchi wananufaika na mpango wa fedha za mikopo kwa vikundi zinazotolewa na Halmashauri zinaongeza tija ndani Halmashauri wilaya Geita imeendelea kuimarisha miradi endelevu ya kiuchumi
Miradi ya maendeleo ndani ya Halmashauri inayosimamiwa na vikundi chini ya uratibu wa Halmashauri ikiwemo ya ufugaji kuku kisasa, kiwanda cha mafuta ya Alizeti cha ushirika Nyabusakama kilichopo kata ya Bugulula vyote vipo katika hatua nzuri.
kiwanda cha mafuta ya Alizeti cha ushirika Nyabusakama kilichopo kata ya Bugulula
Hali hii imefanya kamati ya siasa ya chama cha mapinduzi CCM wilaya wa Geita wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya ndugu Barnabas Mapande kufanya ziara ya kukagua miradi hiyo.
Katika ziara hiyo ndugu Mapande ameridhishwa na muendelezo wa miradi hiyo ya maendeleo ndani ya Halmashauri kusaidia wananchi katika uendeshaji wa miradi hiyo na amewataka viongozi mbalimbali kuwahamasisha wananchi kulima zao la alizeti kwa kuwa soko lipo.
Ziara hiyo ya kamati ya siasa wilaya pia imetembelea katika ujenzi wa kituo cha afya kasota mradi uliokatika ukamilishwaji pia maradi wa mabweni ya kisasa katika shule ya Sekondari Bugando kata ya Nzera pamoja naujenzi wa kisima cha maji safi ndani ya shule hiyo.
Mradi wa ufugaji kuku kisasa
Maradi wa ujenzi wa Mabweni ya Kisasa shule ya Sekondari Bugando kata ya Nzera
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa