Katoro-Geita
Katika Kusheherekea Miaka 4 ya Uongozi wa Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tangu alipo apishwa kuingia madarakani Machi 19, 2021 kufuatia Kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati John Pombe Joseph Magufuli, Watumishi wa umma wametakiwa kuendelea kufanya kazi kwa upendo na uaminifu kuwahudumia wananchi.
Hayo yameelezwa Machi 19, 2025 wakati Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe Hashim Komba alipotembelea Hospitali yenye hadhi ya Wilaya ya Katoro yenye thamani ya shilingi Bilioni 3.7.
Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe Hashim Komba akisalimiana na watumishi katika Hospitali yenye hadhi ya Wilaya Katoro alipofanya ziara kusherehekea Miaka 4 ya Uongozi wa Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe Komba amewataka watumishi hao kuendelea kuwajibika kwa uaminifu na upendo katika kuwahudumia wananchi. “Nitoe Rai kwa watumishi wa kada ya afya kuwa waaminifu na wenye upendo, na kuhakikisha upatikanaji wa vifaa tiba na dawa zinapatikana katika zahanati, vituo vya afya na hospitali ili wananachi wapate huduma” Amesema Mh Komba.
Mhe Mkuu wa Wilaya ya Geita Hashim Komba akipiga rangi Ukuta katika jengo la Hospitali Katoro alipofanya Ziara Machi 19, 2025 Kusherehekea Miaka 4 ya Uongozi wa Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Aidha Mhe Komba amesema Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan imeweka zaidi ya Bilioni 5.6 kwa ajili ya maboresho katika vituo vya afya. “Tunao wajibu wa kumuombea Mhe Rais kwa kazi njema ambazo anaendelea kuzifanya alikuja na kauli mbiu ya kazi iendelee na kweli tumeona namna ambayo kazi njema zimeendelea kufanyika” Ameongeza Mhe Komba.
Ujenzi wa Hospitali ya Katoro umesaidia kupunguza mlundikano wa wananchi wanaokuja kupata huduma kutoka vituo vya afya vya jirani kutoka kata za Lwamgasa, Magenge, Kaseme,Chikobe, Chibingo, Kasamwa, Nyawilomwela, Butundwe.
Baadhi ya Picha Hospitali yenye Hadhi ya Wilaya-Katoro ambayo ujenzi wake unatekelezwa kwa njia ya Force Account ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Geita inanunua vifaa na kuajiri mafundi Mahalia kwa mkataba (Local Fundis)
Hospitali ya Katoro ni matokeo ya ahadi ya aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya Tano Hayati Dkt John Pombe Joseph Magufuli aliposimama kuwasalimia wananchi wa Katoro-Buseresere nakuahidi kutoa shilingi Bilioni 1.5 ambapo Serikali ya Awamu ya sita imeleta kiasi cha shilingi Bilioni 2.2 ikiwa ni kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya wanaume, watoto, wanawake, jengo la kuhifadhia maiti, uzio wa hospitali, nyumba ya mtumishi, usambazaji wa maji, na ujenzi wa jengo la wagonjwa wa dharura (EMD)
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa