Mbunge wa Geita mjini, Mh. Constantine John Kanyasu amepongeza uwepo wa Redio Rubondo huku akisisitiza kuwa imekuwa na mchango mkubwa katika kuhabarisha umma kuhusiana na mambo yanayotokea kwenye jamii.
Akizungumza mwishon mwa juma lililopita katika tamasha la Funga Mwaka na Rubondo FM lililofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Kalangalala Geita Mjini, Mh. Kanyasu amesema kuwa kupitia matamasha yanayoratibiwa na kituo hicho cha redio kila mwaka, Wwananchi wanapata fursa ya kujua shughul mbali zinazofanywa na redio, pamoja na wasikilizaji wake kupata nafasi ya kukutana na watangazaji wao.
"Lengo la kuwa na matamasha kama haya ni kuwapa wasikilizaji fursa ya kupata ujumbe lakini pia kazi zinazofanywa na redio yetu na kuwafahamu watangazaji wetu. Uwepo wa redio hii unatuunganisha na wananchi kwahyo uwepo wenu unafanya kufikika kwa haraka kwa taarifa. Kwahyo niwapongeze kwa hilo." Amesema Mh. Kanyasu.
Mbunge wa Geita Mjini, Mh. Constantine John Kanyasu amekipongeza kituo cha Redio Rubondo, na kuahidi kuendelea kutoa mchango wake ili kulifanya tamasha hilo kuwa bora zaidi.
Aidha, Mb. Kanyasu pia aliahidi kuendelea kuliboresha tamasha hilo kwa kuhakikisha anagawa vifaa vya michezo kwa timu za mpira wa miguu za wanawake na wanaume hapo mwakani ili kutoa nafasi kwa wananchi kujitokeza zaidi na kushiriki katika michezo.
Meneja Masoko kutoka taasisi ya Fedha ya Gold Micro-Credit, Bi. Diana Gamba amewapongeza waandaji wa tamasha la Funga Mwaka na Rubondo FM, pamoja na kusisitiza kuendelea kushirikiana na kituo hicho cha redio.
Meneja Masoko kutoka taasisi ya fedha ya Gold Micro-Credit, ambao pia walikuwa wadhamin wa tamasha hilo, Bi. Diana Gamba, ametoa salamu za pongezi kwa waandaaji wa tamasha pamoja na kuahidi kuedelea kushirikiana na kituo cha Redio Rubondo ili kuleta matokeo chanya kwenye jamii.
Timu ya Watangazaji wa kituo cha Redio Rubondo FM.
Kwa upande wake Meneja wa Vipindi kutoka Redio Rubondo, Ndg. Garos Riwa amesema kuwa wataendelea kushirikiana na wadau mbali mbali ili kulifanya tamasha hilo kuwa bora zaidi, pamoja na kuwashukuru wasikilizaji na wafuatiliaji waliojitokeza kwenye tamasha hilo.
Baadhi ya Wasanii wa kizazi kipya wakitoa burudani kwa wananchi waliojitokeza kwenye tamasha la Funga Mwaka na Rubondo FM.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa