Mwenge wa Uhuru 2025 Umepokelewa katika viwanja vya shule ya Sekondari-Lwezera ukitokea Mkoani Mwanza.
Akizungumza katika Mapokezi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe Martine Shigela amesema Mwenge utakimbizwa umbali wa KM 653 katika Halmashauri Sita za Mkoa wa Geita.
Aidha Mhe Shigela amesema Mwenge wa Uhuru ukiwa ndani ya Mkoa wa Geita utatembelea jumla ya Miradi 61 yenye thamani ya shilingi Bilioni 164.4 ambapo utatembelea na kuona miradi, kuzindua na kuweka mawe ya msingi.
Kwa upande wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Mwenge wa Uhuru umetembelea Jumla ya Miradi 9 yenye thamani ya shilingi Bilioni 2.8 na umekimbizwa umbali wa KM 85.45 kutoka eneo la mapokezi hadi eneo la Mkesha kata ya Ludete.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita chini ya Mkurugenzi Mtendaji Ndg Karia Rajab Magaro inaendelea kuishukuru Serikali kwa namna ambavyo inaendelea kutoa fedha nyingi za miradi ya maendeleo.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa