Jumla ya wanafunzi 394 wa kidato cha nne shule ya Sekondari Lutozo iliyopo kata ya Katoro Wilayani Geita wamehitimu kidato cha nne wasichana wakiwa 184 na wavulana 210.
Akisoma risala Katika mahafali ya Saba ya Shule hiyo, Mwalimu Revocatus John Malaha ambaye ni mkuu wa Shule hiyo amesema wanafunzi wanaoagwa walianza kidato cha kwanza mwaka 2020 wakiwa 479 kati yao wasichana wakiwa 234 na wavulana 245.
Mahala, alisema, shule hiyo imekuwa ya kwanza Katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita huku akipongeza jitihada za walimu, wazazi, wafanyabiasha pamoja na Mh Benedicto Kigongo ambaye ni diwani wa kata ya Katoro .
Aidha alisema shule hiyo imepata Kibali cha kuanzisha kidato cha tano na sita kwa michepuo ya Sayansi na sanaa.
Akizitaja changamoto, Mkuu huyo wa shule alisema, wanakabiliwa na upungufu wa walimu wa masomo ya Sayansi, tatizo la maji safi na Salama pamoja na ukosefu wa mabweni kwa wanafunzi wanaoshi mbali na mahitaj ya kidato cha tano na sita.
Naye Diwani wa kata hiyo Mhe Benedicto Kigongo amefarijika kwa jinsi wazazi wanavyojitoa kuchangia maendeleo ya shule ya Lutozo.
" Najua changamoto ni nyingi Lakini Serikalini yetu sikivu inayoongozwa na Mh Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kutatua changamoto zilizopo kadri fedha za miradi zinavyotoka kufika kwenye Halmashauri Yetu" alisema Kigongo.
Mgeni rasmi katika mahafali hayo ya saba Kaimu Afisa elimu Sekondari Mwalimu Richard Makoye akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Geita Mh Martini Shigela amewataka wahitimu hao kuwa na utii na nidhamu kwa jamii ili wastawi Kwenye maadili mema. " Mkawe mfano mzuri kwa jamii huku mkiyashika yote mliyoelekezwa na walimu wenu kuendelea kusimamia malezi bora yenye maadili ya Kitanzania" alisema Makoye.
Aidha Katika hotuba yake, Makoye aliwataka wahitimu hao kumtanguliza Mwenyezi Mungu katika maandalizi ya mitihani ijayo na kusimama katika misingi mizuri.
" Serikali itajivunia kuwa na vijana mahiri kuijenga nchi yao na niwatake kuzipambania fursa za masomo ya ufadhili ( Mfuko wa mama Samia ) zinazotolewa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na kuifanya shule hii kuendelea kuwa The Giant school," ili kuendelea kuuletea Mkoa wetu wa Geita sifa,"Alisema Makoye.
Pamoja na kuwatunuku vyeti na zawadi wahitimu hao, Kaimu Afisa elimu huyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa aliweza kuongoza zoezi la Harambee ili kufanikisha ujenzi wa mabweni mawili na bwalo ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Geita ilitoa jumla ya mifuko 20 huku wageni waalikwa wakitoa jumla ya mifuko ya saruji 204 na kiasi cha shilingi 5,350,000
Mahafali hayo yalihudhuriwa na watu mbalimbali wakiwepo waheshimiwa madiwani, watendaji kata, wenyeviti wa vijiji na wakuu wa shule za Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa