Katika kuhakikisha maendeleo yanaongezeka kwa wananchi na mwendo wa kimapinduzi katika Nyanja zote yanakuwa na tija ,Viongozi wa Umma,wakuu wa Idara na taasisi binafsi wamepata elimu na mafunzo maalumu kwa lengo la kutunza maadili na uwajibikaji kwa wananchi.
Mgeni rasmi wa Mafunzo hayo Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel amesema uwepo wa watumishi wachache wasio na maadili katika utendaji unarudisha nyuma chachu ya mafanikio na maendeleo kwa wananchi.
Mhandisi Gabriel ameongeza kuwa maadili kwa watumishi wa Umma yanasaidia kuondoa mgongano wa kimaslahi,kuleta utulivu na amani,kusimamia haki na kudhibiti mianya na viashiria vya rushwa.
Mafunzo ya msingi ya maadili kwa watumishi wa Umma ndani ya Mkoa wa Geita yameongozwa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kanda ya Ziwa chini ya katibu msaidizi sekretarieti ya maadili ya viongozi wa Umma kanda ya ziwa Bwana,Godson kweka na kuweka wazi kuwa watumishi wa Umma ni vyema kuzingatia maadili na kuishi katika ahadi ya Uadirifu.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa