Na: Hendrick Msangi
MADIWANI kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Geita Machi 25, 2024 wamepata mafunzo ya jinsi ya kutumia mfumo wa e-board ambao umetengenezwa kwa ajili ya kurahisisha shughuli za vikao/mikutano katika taasisi ikiwemo utunzaji wa nyaraka pamoja na shughulizi nyingine za taasisi zinazohusiana na vikao kwa kupitia matumizi ya Teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA)
Awali akifungua mafunzo hayo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Mhe Charles Kazungu aliwataka madiwani hao kuzingatia mafunzo hayo kwani Teknolojia imebadilika ili kuweza kuendana na mabadiliko ya Teknolojia ya habari na mawasiliano.
Mwenyekiti wa Halmashauri akifungua mafunzo ya mfumo wa e-board yaliendeshwa na wataalam kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Geita. Mafunzo hayo yatawasaidia madiwani wa Halmashauri kuendesha vikao kidijali
Akiendesha mafunzo hayo, Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ndugu Frank Makonda alisema mafunzo hayo kupitia mfumo wa e-board yatawawezesha watumiaji kuhudhuria na kufanya vikao mbalimabli popote duniani kwa kuandika ujumbe wa maneno (Chating) kuongea (audio) na kwa picha za mjongeo (video conferencing)
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita wakiwa kweye mafunzo ya mfumo wa e-board kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita.
Aidha Makonda alisema mfumo wa e-board ulibuniwa kwa sababu ya mambo mbalimbali ambayo yalijitokeza katika kuendesha vikao ikiwepo gharama za uzalishaji wa kabrasha za vikao na kuwafikia wajumbe, mfumo kuweza kuhudumia idadi kubwa ya wajumbe na kupelekea mahudhurio ya vikao kuwa makubwa, kutumia muda mrefu wa kuandaa vikao , mfumo kuwezesha watumiaji walio mbali kushiriki vikao, pamoja na kuibuka kwa janga la ugonjwa wa korona (COVID 19) ambao wajumbe waliweza kuendesha vikoa pasipo kukutana kuepuka maambukizi ya ugonjwa korona.
Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita wakifuatilia mafunzo ya matumizi ya mfumo wa e-board ili kuwajengea uwezo wa kuendesha vikao vya Halmashauri kidijitali.
Halmashauri imewawezesha madiwani wa kata zote 37 za Halmashauri ya Wilaya ya Geita kupata vishikwambi vilivyo nunuliwa kupitia mapato ya ndani kwa gharama za shilingi 46,020,000 kwa ajili ya kuwasaidia kufanya vikao kidijitali.
Akifunga mafunzo hayo, Mhe Kazungu aliwashurukuru wataalam kwa kuendesha mafunzo mazuri kwa waheshimiwa madiwani na kuwataka Waheshimiwa madiwani kuendelea kufanya mazoezi ya kuutumia mfumo huo ili kuufahamu zaidi ikiwa ni pamoja na kuwataka wataalam wa Halmashauri kuendelea kutoa ushirikiano kwa madiwani ili kuendelea kuwajengea uwezo wa kuutumia mfumo huo.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa