• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Halmashauri ya Wilaya ya Geita

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
        • TASAF
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Maji
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Afya
      • Elimu Msingi
        • Utamaduni
      • Elimu Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Manunuzi na Ugavi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • UKIMWI
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Madini
    • Viwanda
    • Biashara
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Uvuvi
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe.Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Elimu,Afya na Maji
      • UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Wahe.Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Sheria ndogo
    • Mpango mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi/kitaifa
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha

MADIWANI GEITA DC WATAKIWA KUSIMAMIA VIZURI FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELEO KATIKA KATA ZAO

Posted on: May 5th, 2023

Na. Michael Kashinde

Wito umetolewa kwa Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita ambao ndio wenyeviti wa kamati za maendeleo ya kata kuhakikisha wanasimamia kikamilifu fedha zilizotolewa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya Ujenzi wa miundombinu ya Elimu ili fedha hizo zikamilishe kazi hizo kwa ubora na kiwango kilichokusudiwa.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Mhe. Charles Kazungu ametoa wito huo wakati akihitimisha mkutano wa kawaida wa baraza la madiwani wa Robo ya Tatu kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Mei 04, 2023 katika ukumbi wa Halmashauri Nzera, ambapo amewataka madiwani hao kuzisimamia kamati za maendeleo katika kata zao ili fedha hizo zinazoingizwa kwenye akaunti za shule zifanye kazi iliyolengwa na Mhe. Rais.

Mhe. Kazungu ametumia mkutano huo wa baraza la madiwani kumshukuru Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia Halmashauri ya Wilaya ya Geita kiasi cha Tshs. 1, 891, 500, 000/= kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya shule kupitia Mradi wa BOOST, pamoja na kiasi cha Tshs. 1, 788, 250, 000/= ambazo ni fedha kutoka Serikali kuu.

Aidha baraza hilo kupitia Mwenyekiti wake Mhe. Charles Kazungu limeishukuru pia Kampuni ya uchimbaji dhahabu ya BARRICK kwa kutoa ufadhili wa kiasi cha Tshs. 487, 300, 000/= katika sekta ya Elimu kwa ajili ya ujenzi wa Miundombinu ya shule za kidato cha Tano na Sita huku madiwani wakishauriwa kuwajengea mazingira mazuri ya kufanyia kazi watumishi mbalimbali hasa wa idara ya Elimu ili kuongeza ufaulu zaidi.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Geita Ndugu Barnabas Mapande akizungumza katika mkutano huo wa baraza la madiwani ameanza kwa kushukuru kwa kazi kubwa iliyofanywa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambapo kwa kipindi kifupi cha miaka miwili tu, ametoa fedha za kujenga shule nyingi ambazo idadi yake inakaribia idadi ya shule zote zilizokuwepo miaka yote ya nyuma huku zikiwa na ubora wa  hali ya juu.

Aidha ametoa ushauri kwa Halmashauri ya Wilaya ya Geita kuzikarabati shule ambazo zinaonekana kuchakaa ili ziweze kukaribia au kufananafanana na zile zilizojengwa kwa fedha za Mhe. Rais, huku akisisitiza usawa wa walimu katika maeneo yote, licha ya tofauti za kimazingira suala linalopelekea baadhi ya maeneo kukimbiliwa na mengine kukimbiwa na walimu hao.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Adv. John Paul Wanga akizungumza katika baraza hilo la madiwani ameeleza kuwa Halmashauri ina mpango wa kushirikiana na wananchi kuboresha mazingira ya watumishi hasa walimu katika maeneo ya nje ya mji kwa kuwajengea nyumba na kuwapatia samani za ndani ikiwa ni sehemu ya motisha kwao ili waweze kuishi kwa furaha katika mazingira hayo.

Akizungumzia huduma ya matibabu bure kwa wazee Adv. Wanga amelieleza baraza la madiwani kuwa Halmashauri imetoa maelekezo kwa watendaji wa kata zote kubaini na kuwatambua wazee wasio na uwezo, ili kuwaweka katika mpango huo wa kupata matibabu bure ambapo lengo la kuwatambua ni kuwapata wale ambao kweli wanauhitaji huo na hawana uwezo.

Mkutano huo wa baraza la madiwani Kwa kipindi cha robo ya Tatu kwa mwaka wa fedha 2022/2023 umejadili na kupokea taarifa za utekelezaji wa shughuli za kiserikali ngazi ya Halmashauri kwa kipindi cha Januari hadi Machi 2023 ambapo baraza hilo limeazimia masuala mbalimbali ikiwemo kusimamia kikamilifu miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa na Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa  Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Tangazo

  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO KWA VIKUNDI January 23, 2025
  • TANGAZO LA KAZI GEITA DC September 10, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA September 16, 2024
  • Geita Mamlaka za Wilaya na malmaka za miji GP DOM.pdf September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • DC KOMBA ARIDHISHWA NA UTEKEKEZAJI WA MIRADI KUELEKEA MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2025.

    May 06, 2025
  • MEI MOSI YALETA FARAJA KWA MAAFISA TARAFA GEITA.

    May 02, 2025
  • RC SHIGELA AIBUA MATUMAINI MAPYA KWA WATUMISHI MKOANI GEITA.

    May 02, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI GEITA DC LAMPONGEZA MKURUGENZI MTENDAJI KWA KUPATA HATI SAFI

    April 30, 2025
  • Tazama zote

video

DED. WANGA AWATAKIA MTIHANI MWEMA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA WANAOJIANDAA KUFANYA MITIHANI YA TAIFA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Asili ya jina Geita
  • Fursa ya viwanda
  • Fursa ya madini
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA KATI, 2021
  • Vivutio vya Utalii
  • Miradi itakayotekelezwa
  • Miradi inayoendelea
  • Orodha ya wahe.Madiwani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Bofya Hapa Kutuma,Kupokea na Kufuatilia Malalamiko,Mapendekezo,Maulizo na Pongezi Halmashauri ya Wilya ya Geita
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Watumishi Portal
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS)
  • Ofisi ya Rais TAMISEMI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter Widgets

Ramani ya Sehemu

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Geita

    Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita

    Simu: +225 282520061

    Mobile:

    Barua pepe: info@geitadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali na Majibu yanayoulizwa mara kwa mara
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa