Kampuni ya Uchimbaji madini ya Geita (GGML) kwa kushirikiana na Kitengo cha usalama barabarani mkoa wa Geita Julai 31, 2024 imeendesha mafunzo ya usalama barabarani kwa madereva na watumishi Halmashauri ya wilaya ya Geita yaliyoratibiwa na ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita.
Mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri yamelenga kuwakumbusha madereva sheria za usalama barabarani hususani katika barabara za kuingia katika mgodi wa dhahabu wa Geita (GGML) na uendeshaji unaozingatia sheria za usalama barabarani.
Meneja wa Idara ya ulinzi kutoka mgodi wa dhahabu wa Geita (GGML) ndg Sylvester Rugaba amewataka madereva wa serikali kuzingatia usalama wa barabarani na wanyamapori walipo ndani ya hifadhi ya mgodi kwani ulinzi wa wanyampori ni jukumu letu sote kuwatunza kwa kuendesha kwa kufuata alama za barabarani.
Akitoa elimu katika mafunzo hayo ya siku moja, Meneja wa Idara ya ulinzi kutoka mgodi wa dhahabu wa Geita (GGML) ndg Sylvester Rugaba amewaeleza madereva hao kuwa ajali nyingi zimekuwa zikihusisha pia barabara za mgodini kutokana na uvunjaji wa sheria, hivyo utoaji wa mafunzo hayo unalenga hasa kuzuia ajali zisizo za lazima kwa kuhakikisha madereva wanazingatia sheria na taratibu za usalama barabarani.
Rugaba amesema kampuni ya uchimbaji wa madini Geita (GGML) imeamua kuendesha mafunzo kwa madereva katika kuwakumbusha juu ya matumizi salama ya barabara kutumia njia za mgodini na nje ya mgodi ikiwa ni pamoja na ulinzi wa wanyamapori waliopo kwenye hifadhi ya mgodi. “Ni jukumu letu sote kutunza wanyama katika hifadhi ya mgodi kwa kuendesha kwa kufuata alama za barabarani” amesema Rugaba.
Aidha Rugaba amewakumbusha madereva kuwa na vitambulisho na leseni pindi wanapoendesha magari na kuwataka kusimama katika malango kwa ajili ya ukaguzi , kuzingatia maagizo ya kiusalama katika malango yote ya kuingia ili kuepuka matukio ambayo yanaweza kuleta usumbufu kwa madereva pamoja na kutoa ushirikiano kwa kuwasiliana iwapo itatokea dharura.” Kuheshimiana,uadilifu kwa watoa huduma katika mageti ili kutunza usalama na kuacha kujihusisha na vitendo viovu” amesema Rugaba.
Sajenti wa jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani Lucas Rwechungura amewaeleza maderava wa serikali kutambua kuwa Familia zinawahitaji hivyo waongeze umakini kufuata sheria za barabarani huku wakiwa na akili timamu isiyokuwa na bugudha ili wanapoingia barabarani wawe na utulivu
Naye Sajenti wa jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani Lucas Rwechungura amewataka madereva wa magari ya serikali kuzingatia matumizi sahihi na salama ya barabara ikiwa ni pamoja na kufuata sheria zote pindi wawapo barabarani.“Familia zinawahitaji hivyo ongezeni umakini kufuata sheria za barabarani huku mkiwa na akili timamu isiyokuwa na bugudha ili mnapoingia barabarani muwe na utulivu” amesisitiza sajenti Lucas.
Madereva wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita wakifuatilia mafunzo ya usalama barabarani yaliyoratibiwa na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita. Mafunzo hayo yameendeshwa na mgodi wa dhahabu wa Geita (GGML) kwa kushirikiana na Kitengo cha usalama barabarani mkoa wa Geita.
Kwa upande wake mwakilishi kutoka ofisi ya Katibu tawala mkoa, Ndg Geofrey Sweke amewaeleza madereva wa serikali kuzingatia sheria kwa kila wanachokifanya ili kuepuka vihatarishi huku akiwataka kutengeneza mbadala wa kutatua changamoto ambazo watakutana nazo na kusisitiza kufanya matukio yatakayo dhibiti vihatarishi.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Geita Dkt Modest Buchard ambaye ni mganga mkuu wa Halmashauri akifungua mafunzo hayo ya siku moja yaliyokuwa na lengo la kuwakumbusha madereva wa serikali juu ya usalama barabarani katika kutumia njia za mgodi wa dhahabu na nje ya mgodi ili kuepukana na ajali zinazoweza kuzuilika. Wakati huo huo Mwenyekiti wa madereva mkoa wa Geita Steven Kachungwa ameshukuru uongozi wa GGML, Mkoa pamoja na Halmashauri kwa ajili ya mafunzo hayo muhimu kwa madereva kuwataka madereva kuendelea kuzingatia misingi ya maadili ambayo ni usalama, heshima, uadilifu, endelevu na ubora pamoja na kutunza vyombo vya usafiri wanavyovitumia.
Mwenyekiti wa madereva mkoa wa Geita Steven Kachungwa amewasihi madereva kuendelea kuzingatia misingi ya maadili ambayo ni usalama, heshima, uadilifu, endelevu na ubora pamoja na kutunza vyombo vya usafiri wanavyovitumia.
Mwisho madereva walikula kiapo cha kuwa waaminifu katika kutii na kuziheshimu sheria za barabarani.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa