Unguja-Zanziber
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla Leo Aprili 03,2025 amefungua Mkutano Mkuu wa 20 Maafisa Habari, Mawasiliano, Itifaki na Uhusiano Serikalini katika ukumbi wa Mikutano wa New Amani Hotel Zanziber.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla akizungumza na Maafisa Habari, Itifaki na Uhusiano Serikalini katika ukumbi wa Mikutano wa New Amani Hotel Zanziber alipozindua Kikao Kazi cha 20.
Akifungua Kikao Kazi cha 20 Mjini Unguja kwa niaba ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi la Zanziber Mhe Dkt Hussein Ally Mwinyi, Makamu huyo amewataka Maafisa Habari nchini kutoa mrejesho kwa wananchi kwa kazi zinazotekelezwa na Serikali kuelekea Uchaguzi Mkuu.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi (MB) akizungumza na Maafisa Habari Itifaki na Uhusiano Serikalini katika ukumbi wa Mikutano wa New Amani Hotel Zanziber katika Kikao Kazi cha 20
" Taarifa za miradi inayotekelezwa na Serikali zote mbili ziwafikie wananchi kwa wakati ili waweze kufanya tathmini ya taarifa za kina za utekelezaji wa miradi ili waweze kufanya maamuzi kuelekea Uchaguzi Mkuu " Amesema Mhe Hemed Suleiman Abdulla.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Mhe Gerson Msigwa akizungumza katika Kikao Kazi cha 20 katika ukumbi wa Mikutano wa New Amani Hotel Zanziber
Pamoja na hayo Mhe Hemed Suleiman Abdulla amewataka Maafisa Habari kuongeza Juhudi za kutangaza miradi yote inayotekelezwa na Serikali ili kuimarisha utawala bora.
Maafisa Habari Itifaki na Uhusiano Serikalini katika ukumbi wa Mikutano wa New Amani Hotel Zanziber katika Kikao Kazi cha 20
Vilevile Mhe Hemed Suleiman Abdulla ametoa wito kwa Maafisa Habari kuendelea kumuunga mkono Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi anazozifanya kuliongoza Taifa ikiwa ni pamoja na kumuombea dua.
Akihitimisha hotuba yake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema Serikali itaendelea kukamilisha miradi yote ikiwepo mradi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere na Reli ya kisasa ya SGR
Kikao Kazi hicho kimelenga kutoa Mafundo na Mazingativu kwa Maafisa Habari wa Tanzania Bara na Zanzibar na kufanya tathimini kwa kazi zilizofanyika kwa mwaka mzmzima.
Makala zilizowasilishwa ni pamoja na Uzoefu wa vyombo vya habari katika kufanikisha chaguzi zilizopita, Wajibu wa jeshi la polisi katika kufanilisha uchaguzi Mkuu na kuhakikisha usalama wa wananchi na waandishi wa habari watakaoshiriki kwenye kuandika habari za Uchaguzi.
Makala nyingine zilizowasilishwa ni Maadili ya vyombo vya habari na waandishi wa habari wakati wa uchaguzi, Uchaguzi Mkuu wa Rais Wabunge na Madiwani, Wajibu wa Maafisa Habari kutoa taarifa za maendeleo kwa wananchi kupitia vyombo vya habari.
Vilevile makala nyingine ambazo Maafisa Habari, Mawasiliano, Itifaki na Uhusiano Serikalini waliweza zipata ni Fursa zilizopo Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) katika kutangaza habari za maendeleo na matumizi ya takwimu kwa maendeleo endelevu.
Kikao Kazi hicho kitaendelea kwa siku 4 hadi Aprili 6,2025 ambapo kitahitimishwa.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa