Mkuu wa mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel amepongeza Halmashauri ya Wilaya Geita, Mgodi wa GGML pamoja na uongozi wa kata ya Nzera kwa ukamilishaji wa ujenzi wa mabweni, madarasa pamoja na Bwalo katika shule ya secondary ya Bugando.
Ujenzi wa mabweni matatu kwenye shule hiyo umegharimu jumla kiasi cha shilingi milioni 298.5 zikiwemo milioni 11 za mapato ya ndani Halmashauri ya wilaya Geita, Milioni 137.5 za miradi ya uwajibikaji kwa jamii (CSR) na milioni 150 kutoka maradi wa lipa kulingana na matokeo (EP4R).
Baadhi ya majengo ya mabweni ya shule ya sekondari Bugando
Mhandisi Gabriel amesema mabweni hayo yataondoa changamoto ya wanafunzi wanaoishi mbali na shule hasa wanafunzi wa kike ambao njiani wanakumbana na changamoto nyingi pamoja na vishawishi kutokana na umbali mrefu.
“Nimesikia kutetemeka nilipoyaona mabweni haya, kwa sababu wanafunzi hawa wanateseka sana kutembea umbali mrefu, wanafunzi wakike wanapata madhara huko njiani ya ubakwaji pamoja na vishawishi mbalimbali” amesema Mhandisi Gabriel.
Habari picha kutoka katika ufunguzi wa mabweni ya shule ya Sekondari Bugando
Aidha Mkuu wa Mkoa amefungua madarasa 10 kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha tano na cha sita kwenye shule hiyo ya sekondari Bugando ambapo ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 99.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa