Nzera-Geita
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Geita Ndg Karia Rajab Magaro leo Aprili 30,2025 amewasilisha taarifa ya maandalizi ya Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2025.
Ndg Magaro amesema Halmashauri kwa kushirikiana na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi inaendelea na zoezi la maandalizi ya Uchaguzi Mkuu kwa kuhakikisha vitu muhimu vyote vinakamilika.
Pamoja na hayo Ndg Magaro amelieleza Baraza hilo kuwa Halmashauri inaendelea na uhakiki wa vituo vya kupiga kura ambapo hadi sasa kuna jumla ya vituo 490.
"Halmashauri inashirikiana na Tume Huru ya Uchaguzi ili kupata Idadi halisi ya wapiga kura wenye vitambulisho vya kupiga kura kutoka Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ili kujua idadi ya vituo vitakavyozalishwa." Amesema Ndg Magaro.
Kuhusu maandalizi ya uboreshaji wa daftari la Mpiga kura awamu ya pili, Mkurugenzi Mtendaji Ndg Magaro amesema zoezi hilo litaanza Aprili 01, 2025 hadi Aprili 07, 2025 katika vituo 45.
"Niwaombe Waheshimiwa Madiwani kuwahamasisha wananchi ambao hawajaandikishwa kuwa na vitambulisho kwa ajili ya kupiga kura kujitokeza ili waweze kupata haki ya Msingi na ya kidemokrasia kuwachagua viongozi wao." Amesema Ndg Magaro.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Mhe Hadija Said ametoa rai kwa Waheshimiwa Madiwani kufanya mikutano na wajitokeze katika uboreshaji wa daftari la Mpiga kura awamu ya pili linalotarajiwa kuanza Mei Mosi na kumalizikia Mei 7, 2025.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita ina jumla ya kata 37 na majimbo mawili ya uchaguzi ambapo mchakato wa kugawa Jimbo la Busanda unaendelea.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa