Halmashauri ya Wilaya ya Geita imetumia kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 400 ili kuiboresha na kuipandisha hadhi iliyokuwa zahanati na sasa kituo cha afya Kasota kama sehemu ya mpango wa kuboresha huduma ya afya kwa Jamii.
Akizungumza katika ufunguzi wa kituo hicho Mganga Mkuu wa Wilaya ya Geita Daktari Deo Kisaka amesema uboreshwaji wa miundombinu na manunuzi ya vifaa tiba vya kisasa utaongeza ufanisi wa huduma
Dokta Deo Kisaka ameongeza kuwa huduma muhimu katika kituo hicho ikiwemo jingo la upasuaji,wodi ya kulaza wagonjwa ,wodi ya mama na mtoto pamoja na nyumba za watumishi itawanufaisha wakazi zaidi ya elfu 9 ndani ya kata 4 za jirani.
Kwa upande wake Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita bwana Dornad Nsoko anaamini zaidi ya vijiji 130 ndani ya Halmashauri ya wilaya vitapata huduma ya afya na vifaa tiba kwa wakati
Mkuu wa mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel ambae amezindua kituo hicho amesema kama mkoa hawatakaa kimya kwa mtu anae jihusisha na vitendo vya kukwamisha miradi ya maendeleo ndani ya Mkoa na kuwataka viongozi kuwa na mipango mizuri katika kuisimamia miradi ya jamii inayotekelezwa kwa fedha za wananchi.
Huku wananchi wa Kasota wakiamini kuongezeka kwa huduma kutapunguza gharaza za kusafiri umbali mrefu kupata tiba kitendo kilichokuwa kinagharama kubwa .
Ujenzi wa kituo hicho ni ushirikiano wa Mapato ya ndani ya halmashauri ya Wilaya pamoja na fedha za uwajibikaji wa makapuni kwa jamii kitoka mgodi wa dhahabu Geita katika upande wa vifaa tiba ndani ya kituo hicho cha Afya
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa