Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Geita leo Novemba 13, 2024 limekutana katika Mkutano wake wa kawaida wa robo ya kwanza katika mwaka wa fedha 2024/25.
Katika Kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri -Nzera, Waheshimiwa Madiwani wamewasilisha taarifa za utekelezaji wa Shughuli za Serikali ngazi ya Kata kwa kipindi cha mwezi Julai hadi Septemba 2024.
Jumla ya Kata 37 za Halmashauri ya Wilaya ya Geita zimewasilisha taarifa za utekelezaji wa Shughuli za Serikali katika robo ya kwanza.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Mhe Charles Kazungu akizungumza na madiwani (Hawamo pichani) katika kikao cha kwanza cha robo ya kwanza ya mwaka 2024/2025 kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri Nzera. picha na kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
Akizungumza katika Baraza hilo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Mhe Charles Kazungu ambaye pia ni Diwani wa kata ya Butobela amewasihi Waheshimiwa Madiwani hao kuendelea kusimamia utekelezaji wa Shughuli za Serikali kwa kuendelea kushirikiana na Watendaji ili Shughuli za Serikali zikamilike kwa Wakati.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Geita Bi Sarah Yohana amesema Halmashauri kupitia bajeti zake itaendelea kutatua changamoto mbalimbali ambazo waheshimiwa Madiwani wameziwasilisha katika Baraza hilo.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa