Katibu Tawala Mkoa wa Geita Ndg Mohamed Gombati, Septemba 25, 2024 amewataka walimu kuendelea kuzingatia maadili na miiko ya kada ya ualimu ili kuendelea kuuletea Mkoa wa Geita sifa njema.
Gombati ameyasema hayo katika hafla ya Kuwapongeza walimu wa shule za Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Geita kwa shule zilizofanya vizuri katika mitihani ya kitaifa kidato cha pili, cha nne na cha sita.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Geita Ndg. Mohamed Gombati (katikati) akizungumza na wakuu wa Shule za sekondari, wadau wa elimu na wanafunzi waliohudhuria hafla ya utoaji tuzo iliyofanyika Geita Mjini. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Geita Ndg. Karia Magaro na kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Charles Kazungu.
Walimu hao wametakiwa kuendelea kutoa ushirikiaono baina yao wenyewe, wazazi na Viongozi ili kuendelea vizuri zaidi. " Mafanikio haya yemetokana kwa namna ambavyo Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anavyoboresha maslahi ya walimu ikiwa ni pamoja na miundombinu, hivyo nitoe rai kwenu kuendelea kushirikiana pamoja na kusimamia maadili ya Wanafunzi wetu kuwajenga katika nidhamu ili waheshimu maadili wanayojifunza" amesema Gombati.
Walimu wa shule za Sekondari, wadau wa elimu na wanafunzi wakiwa katika Hafla ya utoaji tuzo kwa shule zilizofanya vizuri katika mtihani wa kidato cha pili, kidato cha nne na kidato cha sita.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Mhe Charles Kazungu amewataka Wakuu wa shule, Maafisa Elimu kuendelea kuongeza bidii na kutokubweteka na ufaulu wa sasa.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Ndg. Charles Kazungu akizungumza na wakuu wa shule za Sekondari wadau wa elimu na wanafunzi katika Hafla ya ugawahi tuzo kwa shule zilizofanya vizuri.
"Sisi Halmashauri ya Wilaya ya Geita tuna asilimia 40 ya shule kimkoa, hivyo tukifanya vizuri tunauinua Mkoa wetu wa Geita" amesema Mhe Kazungu.
Vile vile Mhe Kazungu amewahakikishia walimu hao kuendelea kutoa motisha kwa kuendelea Kuwapongeza ili kutoa chachu ya kuendelea kufanya vizuri.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya na Maji Halmashauri ya Wilaya ya Geita ambaye pia ni Diwani wa kata ya Nyaruyeye Mhe Malimi Samson amesema taarifa za ufaulu zinaleta faraja na kusema Halmashauri itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya kutoa motisha kwa walimu na Wanafunzi wanaofanya vizuri.
Diwani wa kata ya Nyaruyeye Mhe. Malimi Samson Akizungumza katika hafla ya utoaji tuzo
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Geita ndg Karia Rajabu Magaro amewapongeza walimu kwa kuongeza asilimia ya ufaulu na kusema Halmashauri itaendelea kuboresha bajeti zake ili kuendelea kuwapa motisha walimu na Wanafunzi.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Geita Ndg. Karia Magaro akizungumza katika hafla ya utoaji tuzo.
Pamoja na hayo Afisa Elimu Sekondari Mwalimu Hosanna Nshulo amesema Halmashauri kwa kushirikiana na Serikali Kuu na Sekta binafsi imeweza kuongeza na kusajili shule mpya 29 za Sekondari za Serikali na Shule 2 mpya za Sekondari zisizo za Serikali kwa kipindi cha mwaka 2022 hadi 2024.
Afisa Elimu Sekondary Mwl Hosiana Nshulo akitoa taarifa ya hali ya elimu katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Nshulo ameongeza kwa kusema Serikali inayo ongozwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan imeleta fedha kwa ajili upanuzi wa shule 2 za Sekondari ili kuwa na kidato cha 5 na 6 na kufanya Halmashauri kuwa na shule za Sekondari 77 kwa kidato cha kwanza hadi cha nne na shule 4 zinazotoa Elimu ya Sekondari ya juu hali ambayo imechangia kuinua kiwango cha taaluma shuleni na ufaulu kwa ujumla.
Baadhi ya watumishi mbalimbali wakitunukiwa
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa