Jumla ya watu 8341 waliopima ugonjwa wa UKIMWI katika Halmashauri ya wilaya ya Geita ndani yamiezi 10 mwaka huu wamepatikana na UKIMWI
Takwimu hizo zimetolewa na mratibu wa UKIMWI katika halmashauri ya wilaya ya Geita Patricie Nsinde wakati wa maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani yaliofanyika Disemba 1 katika kijiji cha Bugalama mkoani Geita ambapo waliopima walikuwa zaidi ya lakimoja na 8,341 ndiyo wamepatikana na maambukizi.
Katika taarifa hiyo takwimu za maambukizi ya virusi vya UKIMWI na magonjwa ya ngono jumla ya watu waliopima katika kipindi cha mwezo Januari hadi Oktoba 2019 ni 116,340 kati ayo waliogundulika kuwa na VVU ni 86641 (Me 3,316 na Ke 5325 ) sawa na asilimia 7.4 kiwango hiki ni kimeongezeka kwa asilimia 1.8ikilinganishwa na takwimu za mwaka jana ambapo maambukizi yalikuwa ni sawa na asilimia 5.6
Katika majadiliano hayo ya pamoja katika siku hii ya UKIMWI duniani hali inaonyesha wanawake ndio waathirika zaidi hali inayotajwa na wataalamu wa afya kusababishwa na maambukizi sugu ya magonjwa ya ngono kama Kaswende yanayoshambulia via vya uzazi.
Utafiti wa kitalaamu unazitaja changamoto za,Ushamili wa maambukizi mapya kwa vijana,Mwitikio mdogo wa wanaume kujitokeza kupima VVU,Uhaba wa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa afua za kupambana na UKIMWI pamoja na uhaba wa wataalam wa idara ya afya ndio chanzo cha kuongezeka kwa maambukizi ya VVU.
Katika hatua nyingine kwa kipindi cha kuanzia Januari hadi Oktoba 2019 ,Halmashauri ya Wilaya ya Geita imefanikiwa kutumia shilingi za Tanzania 5,000,000/= kuwezesha watu wanaoishi na VVU kutekeleza majukumu yake Vilevile kiasi cha shilingi za Tanzania 5,772,000/= zimetumika kuhudumia watoto 84 yatima na wanaoishi katika mazingira tete.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa