Na: Hendrick Msangi
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Itikadi, Uenezi na Mafunzo Cde. Paul Makonda amezitaka kamati za siasa Wilaya na Mkoa kushirikiana kuwabana watendaji wote kwenye Halmashauri zote ambao wanakwamisha shughuli za kiutendaji katika maeneo yao.
Hayo yameelezwa Novemba 11, 2023 Mkoani Geita, wakati Paul Makonda alipokuwa kwenye mkutano wa hadhara kwenye moja ya ziara zake ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Cde Makonda alisema kamati za siasa zisiwavumilie watumishi ambao wamekuwa ni chanzo cha migogoro kwenye jamii, watumishi ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya rushwa katika miradi mbalimbali ambayo serikali inayoongozwa na Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatenga kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya kuwaletea wananchi maendeleo kwa kuhakikisha Miradi yote inatekelezwa kwa uaminifu na kwa wakati.
“Wapo baadhi ya watumishi wasio waaminifu, chukueni hatua kwa watumishi wote wanaorudisha maendeleo nyuma kwani Mhe. Rais anatoa fedha nyingi kwa ajili ya miradi kwenye halmashauri zote na fedha hizo zielekezwe sehemu husika,” alisema Cde Makonda.
Aidha katika Mkutano huo , Cde Makonda aliwashukuru wananchi wa mkoa wa Geita kwa upendo na maombi yao kwake ili aendelee kuwa msemaji wao na aliwataka wananchi hao kuendelea kuiunga mkono na kuiamini serikali yao inayoongozwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita inaendelea kuishukuru serikali kwa kuendelea kutenga fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa