Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi kata ya Butobela imemshukuru na kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuiletea kata hiyo kiasi cha Shilingi milioni 160 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba nane vya madarasa katika shule ya Sekondari Butobela.
Kamati hiyo imetembelea Mradi huo wa ujenzi wa vyumba nane vya madarasa Disemba 23, 2021 na kusema Mradi huo utasaidia kuondoa changamoto mbalimbali za Elimu.
Mwenyekiti wa kamati hiyo Pius Matongo Jolijo amempongeza Rais Samia kwa kuikumbuka kata hiyo ya Butobela na kuipatia kiasi hicho cha shilingi milioni 160 kwa ajili ujenzi wa vyumba vya madarasa hayo huku akisema kuwa wao wanamuunga mkono Rais Samia katika kila hatua ya utekelezaji wake wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM.
Aidha kamati hiyo ya Siasa imeeleza kuridhishwa kwake na maendeleo ya Mradi huo wa vyumba nane vya madarasa ambao uko katika hatua za ukamilishaji huku Mwenyekiti wake Pius Mtaongo Jolijo akitoa wito kwa jamii kuwapeleka watoto shuleni Januari mwakani kwa kuwa tayari Rais Samia kaboresha mazingira.
Ujenzi huo wa vyumba nane vya madarasa katika shule ya Sekondari Butobela ni miongoni mwa jumla ya vyumba 352 vya madarasa vinavyoendelea kujengwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita kupitia fedha za tozo za miamala ya simu na mpango wa UVIKO
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa