Kamati ya Siasa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilayani Geita imempongeza Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Geita kwa Usimamizi mzuri wa Fedha za Miradi ya Maendeleo.
Hayo yameelezwa katika Ziara ya Siku mbili Januari 9 na10, 2025 iliyofanywa na Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake Komredi Barnabas Mapande katika jimbo la Busanda na Geita.
Mapande ameipongeza ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Geita kwa kusimamia vema fedha za miradi zinazoletwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kamati hiyo ikiwa katika Hospitali ya Wilaya kata ya Nzera ambapo imetembelea ujenzi wa Uzio wa Ukuta wenye thamani ya Shilingi Milioni 225,000,000 imesema Uzio huo ni muhimu kwa Hospitali hiyo ili kuweka mazingira mazuri yenye utulivu na usalama kwa Watumishi na hata wagonjwa kutoka Sehemu mbalimbali wanaofika Kupata huduma katika hospital hiyo.
Ujenzi wa Uzio katika Hospitali ya Wilaya Nzera wenye thamani ya Shilingi Milioni 225,000,000. Ujenzi wa uzio huo utasaidia kuongeza usalama wa mali za Hospitali na watumishi wake na kuboresha mazingira ya utendaji kazi.
Akizungumza mbele ya Kamati ya Siasa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt Shadrack Omega amesema kukamilika kwa Uzio huo kutapelekea mazingira mazuri kwa watumishi wa Hospitali pamoja na wagonjwa wanaofika Kupata huduma katika hospital hiyo.
“Kulikuwa na matukio ya wagonjwa kutoroka, wengine kung'atwa na mbwa na wakati mwingine mifugo kuingia katika eneo la hospitali ila kwa sasa Uzio utakuwa suluhu" amesema Dkt Shadrack Omega.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya-Nzera Dkt Shadrack Omega akizungumza mbele ya Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilayani Geita ambapo ameishukuru Serikali inayoongozwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha ujenzi wa Uzio wa Hospitali hiyo inayohudumia wananchi kutoka maeneo mbalimbali
Kamati hiyo imemtaka fundi anaye jenga uzio huo kuendelea na Kasi ya ujenzi ili ukuta huo ukamilike haraka na kuepusha adha mbalimbali zilizo kuwa zinajitokeza katika Hospitali hiyo ya Wilaya.
Ujenzi wa ukuta wa Hospitali ya Wilaya –Nzera unatarajiwa kukamilika Machi 10, 2025 ambapo mpaka sasa asilimia za utekelezaji ni 45% ukijumuisha nyumba ya mlinzi na uzio(fence)
Mwenyeki wa Chama Cha Mapinduzi Wilayani Geita Komredi Barnabas Mapande (Aliyeshika kipaza sauti) akiwa na wajumbe wa Kamati ya Siasa Wilaya katika Ziara ya Kukagua Miradi ya Maendeleo katika Hospitali ya Wilaya-Nzera ikiwa ni sehemu ya Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Halmashauri ya Wilaya ya Geita inaendelea kuishukuru Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa nia yake njema kutoa fedha nyingi kwa ajili ya miradi ikiwa ni pamoja na ujenzi wa uzio ili kuwezesha usalama wa hospitali na kuboresha mazingira ya kazi,
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa