Kamati ya fedha uchumi na Mipango Halmashauri Wilaya Geita yalidhishwa na maendeleo ya ujenzi wa miradi mbali mbali iliyo katika utekelezwaji.
Katika kuhakiksha maendeleo ya wananchi yanakuwa kwa kasi na huduma zake zinakuwa zenye manufaa, Kamati ya fedha Uchumi na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya Geita imezuru katika kata mbalimbali na vitongoji vyake kukagua maendeleo ya Miradi iliyo katika mipango ya Halmashauri.
Katika ziara hiyo iliyoongozwa na Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Bi.Khadija Said akiambatana na madiwani kadhaa na wajumbe kutoka idara husika wamefanikiwa kukagua mradi wa Maji Chankorongo uliofungwa pump kuhudumia vijiji vitano, huku gharama za ununuzi wa vifaa hivyo ukitajwa kugharimu kiasi cha zaidi ya Shilingi Milioni 21.
Pia Kamati hiyo imefika kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa na maabara shule ya Sekondari Nyankogochoro kata ya Lubanga, unaotarajiwa kukamilika siku chache zijazo hali inayoleta matumaini ya kuongezeka kwa ubora wa miundombinu ya Elimu na ufaulu kwa masomo ya sayansi.
Mbali na Miradi hiyo Kamati imeweka wazi juu ya mpango wa kujenga Stend ya kisasa ya Mabasi kata ya Katoro eneo lenye ukubwa wa Heka 44.7 na kazi hiyo itaanza mara baada ya kukamilika tathimini ya mradi huo.
Vituo vya Afya na Zahanati zilizopo ndani ya Halmashauri wilaya ya Geita vimekuwa sehemu ya ukaguzi wa kamati, huku ikionyeshwa kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa majengo manne ya kituo cha afya Nyarugusu unaogharimu kiasi cha Shilingi Milioni 400 kama sehemu ya kuimarisha huduma za afya.
Licha Halmashauri kutoa Fedha ndani ya kata na vijiji ili kuongeza ufanisi wa Miradi lakini bado imebaini kuwa sehemu kubwa ya jamii haina Muamko wa ushiriki katika maendeleo hasa huduma za Afya na Elimu.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa