Jamii imetakiwa kuendeleza mapambano dhidi ya virusi vya UKIMWI kwa kuchukua tahadhari zote na kupima Afya mara kwa mara ili kufahamu hali zao na kuzuia maambukizi mapya ya VVU
Disemba Mosi 2021 katika maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani Mkuu wa Wilaya ya Geita Mheshimiwa Wilson Shimo akiwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo yaliyofanyika ki Wilaya katika viwanja vya CCM Nkome katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita alitoa wito huo.
Mheshimiwa Shimo alisema kuwa kila Mwananchi anatakiwa kulinda Afya yake kwa kupima VVU na kuchukua tahadhari zote huku akitoa wito wa kuhamasika kupata chanjo ya Uviko 19 na kushiriki katika zoezi la Sensa linalotarajiwa kufanyika mwakani 2022.
Awali akitoa taarifa kwa mgeni rasmi Mratibu wa UKIMWI katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita Bi.Patricia Nsinde alisema kuwa kiwango cha maambukizi kimeongezeka kwa asilimia 5.9 ukilinganisha na takwimu za mwaka jana ambapo maambukizi yalikuwa sawa na asilimia 5.6
Miongoni mwa changamoto zilizobainishwa katika taarifa hiyo ni pamoja na mwitikio mdogo wa wanaume kujitokeza kupima VVU huku maambukizi yakishamiri zaidi kwa kundi la vijana.
Miongoni mwa mikakati iliyowekwa na Halmashauri ya Wilaya ya Geita katika kukabiliana VVU ni pamoja na kutoa Elimu kwa jamii kuhusu UKIMWI, kuunda klabu za UKIMWI katika shule za msingi na sekondari, kuboresha huduma za upimaji wa VVU, na kurahisisha upatikanaji na usambazaji wa kondomu kwa wahitaji.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa