Nyakamwaga-Geita DC
Na: Hendrick Msangi
Operesheni ya kukagua miradi ya maendeleo na kusikiliza kero za wananchi Halmashauri ya wilaya ya Geita kwa kata 9 imekamilika kwa awamu ya kwanza ambapo Mhe Hashim Komba akiwa na kamati ya ulinzi na usalama, Wakuu wa Idara na Vitengo pamoja Taasisi za serikali ikiwepo TANESCO, TAKUKURU, RUWASA na TARURA wameshiriki zoezi hilo.
Ziara hiyo imehitimishwa kwa kutembelea miradi ya maendeleo kwa vijiji 7 vya Kata ya Nyakamwaga ambavyo ni Iponyamakalai, Buyagi,Bufunda,Kashishi, Ihemelo, Kasongamile na Nyakamwaga
Ujenzi wa vyumba 3 vya madara Shule ya Msingi Iponyamakarai kwa nguvu za wananchi kwa kiasi cha shilingi milioni 18 ambapo wananchi hao wamemuomba Mkuu wa Wilaya kuweka msukumo ili vikamilike. Aidha wazee wa kijiji hicho wameishukuru Serikali kwa kupokea kiasi cha shilingi 29,854,000 kwa kuwezesha kaya masikini 53
Katika operesheni hiyo Mhe Komba ameendelea kuwasisitiza watumishi wa umma kuwa na uchungu katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kutoa onyo kali kwa watumishi wa umma na wakandarasi watakaokwamisha miradi.” Tuwe na uchungu wa kusimamia wadau wa maendeleo ili miradi iwe na thamani ya fedha zinazoletwa na serikali.” Amesema Mhe Komba.
Ukamilishwaji wa mradi wa Zahanati ya kijiji cha Bufunda kata ya Nyakamwaga. Mradi huo uliibuliwa mwaka 2016 na kuanza kutekelezwa mwaka 2017 huku hatua za uchimbaji hadi boma zikifanywa na wananchi kwa gharama ya shilingi 9,982,000 na hatua za uwezekaji zikifanywa na Halmashauri kupitia mfuko wa CSR kwa kutoa vifaa vya ujenzi na malipo ya mafundi.
Mradi wa Zahanati ya Ihemelo ulianzishwa mwak 2019 na kugharimu kiasi cha shilingi 17,800,000 ambapo kiasi cha shilingi 10,000,000 ni mapato ya ndani ya Halmashauri na shilingi 7,800,000 kutoka nguvu za wananchi. Zahanati hiyo ikikamilika itawanufaisha wazee , watoto na mama wajawazito kwa kupunguza umbali wa kufuata huduma za afya.
Aidha amewataka watumishi wa umma kuzitumia nafasi walizo nazo kuwasaidia wananchi kwa kushuka chini kuwasikiliza kero na changamoto walizo nazo wananchi na kuzitatua kwa kuzingatia haki na wajibu ili kuepuka migogoro mbalimbali kutoka kwa wananchi badala ya kuwasubiria viongozi wakubwa kufika kutatua kero zao.
Ujenzi wa daraja la mlamaki (4mx2m) barabara ya Kagu-senga na daraja la kasungamile (2mx2m) barabara ya katoro-nyabulolo-nyalwanzaja unaotekelezwa na mkandarasi Samma Estate Limited kwa gharama ya shilingi 145,001,350. Mradi huo unatarajiwa kukamilika ifikapo August 22, 2024 ambapo shughuli za usimamizi wa daraja hilo zinafanywa na Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini (TARURA)
”Nataka nione watumishi wa umma wanaosikiliza kero za wananchi. Nafasi tulizo nazo leo haimaanishi kwamba sisi ndio watu muhimu sana kuliko watu wengine , ukiona wewe ni mtendaji wa kijiji au kata jua kabisa wapo watu wengine wana sifa za kuwa watendaji wa vijiji au kata lakini hawajapata nafasi .”amesisitiza Mhe Mkuu wa Wilaya.
Ujenzi wa nyumba ya mtumishi pacha Zahanati ya Nyakamwaga wenye thamani ya shilingi 53,239,152 ambapo nguvu za wananchi ni kiasi cha shilingi 1,500,000, Mapato ya ndani shilingi 10,000,000, mfuko wa CSR shilingi 41,739,152
“Huwa nina waambia watumishi wa umma wenzangu unaweza ukawanyanyasa watu kwa kupokea rushwa na kujipatia fedha nyingi ila wakati una staafu tuu Mungu ana namna yake ya kuhangaika na machozi ya watu ulio wanyanyasa kwa kuwadhulumu haki zao wanapomlilia Mungu utashangaa mara unapata kisukari, magonjwa ya presha hata kuparalaizi unaanza kutumia zile hela ambazo uliwadhulumu wananchi kwa nafasi uliyopewa kuwatumikia.” Ameongeza Mhe Komba
Mhe Mkuu wa Wilaya ya Geita Hashim Komba akiwa na Diwani wa Kata ya Nyakamwaga Mhe Thomas Kayange (Aliyevaa Kofia) wakaki alipofanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo katika kata hiyo
Mwisho amewataka wananchi hao kuendelea kudumisha amani na utulivu kwa kuwa taifa limejengwa katika misingi ya upendo na kuendelea kuiamini serikali inayo ongozwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa