Naibu waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Dr.Anjelina Mabula ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Geita kwa kutenga kiasi cha shilingi milioni 300 kwa ajili ya idara ya ardhi suala linalorahisisha utendaji wa idara hiyo.
Ametoa pongezi hizo akiwa katika ziara ya kikazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita baada ya kupewa taarifa ya idara hiyo,ambapo amesema kuwa ni Halmashauri chache sana hapa nchini zinazoweza kutenga fedha kiasi hicho kwa ajili ya idara ya Ardhi huku akisema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Geita ni mfano wa kuigwa kwa hilo.
Amewataka watumishi wa idara hiyo kubuni mbinu za kudhibiti ujenzi holela huku akishauri kuwatumia wenyeviti wa vijiji na watendaji kwa ajili ya kupata taarifa na kuhoji kwa watu wanaoanza ujenzi kama wamepata vibali suala litakalosaidia kuipanga miji.
Aidha amewataka watumishi wa idara ya Ardhi kuongeza kasi ya kupima viwanja na kugawa hati, sambamba na kutoa elimu ya faida za kupimiwa maeneo suala litakalowahamasisha wananchi kuchangamkia fursa ya kupimiwa maeneo yao kuliko kuogopa.
Wakati huo huo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita John Paul Wanga ameahidi kufanya kazi na idara hiyo ambapo ndani miezi mitatu na wiki mbili atahakikisha viwanja vyote vinaingizwa kwenye mfumo,suala litakalosadia kuiongezea Serikali mapato.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa