Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita limemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuitengea Halmashauri hiyo ya Wilaya ya Geita bilioni 7 na milioni 940 kutoka Fedha za Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo ya Ustawi na Mapambano Dhidi ya Uviko 19 kwa ajili ya Miradi ya Elimu na Afya.
Akizungumza kwa niaba ya Baraza hilo siku ya pili ya mkutano wa kawaida wa baraza la Madiwani wa robo ya kwanza kwa mwaka wa fedha 2020/2021 Novemba 12, 2021 Diwani wa kata ya Isulwabutundwe Mheshimiwa Maweda Gwesandili.
Ametoa shukrani hizo huku akisisitiza ushirikiano wa karibu katika usimimizi wa Miradi itakayotekelezwa kupitia fedha hizo.
Awali taarifa ya Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo ya Ustawi na Mapambano Dhidi ya Uviko 19 iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita John Paul Wanga ilieleza kuwa Mikakati yote iliyowekwa katika kikao cha Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Geita cha Tarehe 20/10/2021 imetekelezwa ikiwemo uteuzi wa kamati mbalimbali za usimamizi.
Kamati hizo zimepewa jukumu la kusimamia Miradi hiyo kwa ukaribu na kutoa taarifa za haraka kwa mamlaka za juu pale zinapokumbana na changamoto zozote katika kutekeleza majukumu hayo ili kuharakisha ujenzi wa Miradi hiyo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Geita Barnabas Mapande yeye amesema kuwa wao kama Chama wana Jukumu la kufuatilia na kuona namna fedha hizo zinavyofanya kazi hivyo ametoa wito wa kuandaa taarifa zenye mchanganua wa matumizi ya fedha hizo kwa usahihi huku akiahidi kuwawajibisha watakaozitumia kwa maslahi yao binafsi.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa