Halmashauri ya Wilaya ya Geita imeamua kuunda kamati za ufuatiliaji, ujenzi, manunuzi na mapokezi kwa ajili ya kuratibu shughuli za ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo ili kuongeza ufanisi katika kutekeleza miradi hiyo.
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita wakiendelea na Mkutano
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita John Paul Wanga akiwa katika mkutano maalumu wa baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Oktoba 5 2021, wa kujadili mapendekezo ya mpango na bajeti ya CSR wa mwaka 2021 amesema kuwa timu ya menejimenti imeamua kufanya hivyo kwa kuwa Halmashauri ni kubwa na ina upungufu wa Wahandisi.
Amesema kuwa kamati hizo zitafanya kazi kwa mgawanyo wa majukumu kama zinavyojieleza ambapo kamati ya manunuzi itanunua vifaa vitakavyopokelewa na kamati ya mapokezi, huku Mhandisi na Mtendaji wakiongoza kamati ya ujenzi ambapo pia Diwani wa kata yenye mradi ndio atakuwa Mwenyekiti wa kamati ya ufuatiliaji.
Mbunge wa Jimbo la Busanda (wa kwanza kushoto aliyesimama) Mh.Tumaini Bryson Magesa akizungumza katika mkutano maalumu wa Baraza la Madiwani,(katikati)Mh.Charles Kazungu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita,(wa kwanza kulia)Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita John Paul Wanga
Ameendelea kusema kuwa ameagiza kila kamati iwe na mwanamke ambaye ni Mwanajamii wa sehemu yenye mradi kwa kuwa Mama zetu ni waaminifu sana na hawawezi kurubuniwa kwa urahisi suala litakalopunguza malalamishi yaliyokuwepo ya kuanzisha miradi lakini haifiki mwisho.
Aidha amesema kuwa atahakikisha wanafanya haraka ili wasaini Mkataba wa CSR na Kampuni ya GGML huku akiahidi kufuatilia utekelezaji wa miradi hiyo katika kila hatua na kuwataka Madiwani wa kata husika kufanya hivyo pia.
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita wakiendelea na Mkutano
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa