Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Geita Mwl.Edith Mpinzile, ametoa wito kwa Makampuni,Mashirika,Taasisi,na wadau mbalimbali wa maendeleo mkoani Geita, kujitokeza kusaidia miradi ya elimu hasa ujenzi wa nyumba za walimu, katika maeneo ambayo hakuna hata nyumba za kupanga.
Ametoa kauli hiyo leo Agosti 18 alipokuwa akizungumza na Afisa mawasiliano Mwandamizi wa kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML), Bw.Laurian Theophil Pima, ambapo amesema kuwa kuna changamoto kubwa ya uhaba wa nyumba za walimu, hasa kwenye maeneo ambayo hakuna nyumba za kupanga.
Amesema kuwa Mwalimu anahitaji kuheshimiwa na kuthaminiwa, ili awe na afya nzuri ya mwili na akili aweze kuzalisha watoto bora.hivyo, ni vyema akajengewa mazingira mazuri, ili afanye kazi zake kwa ufanisi, na hatimaye tupate matokeo mazuri tunayoyategemea.
Kaimu Mkurugenzi Wa Halmashauri ya wilaya ya Geita Mwl.Edith Mpinzile akizungumza ofisini kwake na Afisa Mawasiliano mwandamizi Wa GGML Bw.Laurian Theophil Pima
Akinukuu kauli mbiu inayopendwa kutumiwa na mkuu wa mkoa wa Geita Bi.Rosemary Senyamule ya “GEITA YA DHAHABU, UTAJIRI NA HESHIMA” Mwl.Mpinzile amesisitiza kuwa, utajiri na heshima vitaonekana, pale wadau watakapojitolea kusaidia miradi ya maendeleo, na kuzalisha wataalamu wa baadae tuliowaandaa wenyewe.
Aidha ameipongeza kampuni ya Geita Gold Mining Limited, kwa mchango wake mkubwa katika maendeleo ya elimu na miradi mingine,ambapo kampuni hiyo imesaidia kujenga vyumba vitatu vya madarasa kwa ajili ya kidato cha tano na sita, mabweni matatu,bwalo la chakula,na kisima cha maji katika shule ya sekondari Bugando kupitia mradi wa fedha zinazotolewa na kampuni kama wajibu wake Kwa jamii yaani CSR.
Madarasa matatu ya A level yaliyojengwa na GGML kupitia mradi CSR katika Shule ya sekondari Bugando iliyopo ndani ya Halmashauri ya wilaya ya Geita
Mabweni matatu yaliyojengwa na GGML kupitia mradi wa CSR Kwa ajili ya wanafunzi Wa A level katika Shule ya sekondari Bugando.
Kwa upande wake makamu mkuu wa shule ya sekondari bugando mwl.Gibson Petro ameishukuru GGML kupitia mradi wa CSR, kwa kuwasaidia katika ujenzi wa miradi hiyo huku akieleza kuwa kuanzishwa kwa masomo ya kidato cha tano na sita shuleni hapo kumeongeza hamasa na bidii kwa wanafunzi wa madarasa ya chini ambao wanaonekana kuwa na shauku pia ya kuendelea na masomo ya kidato cha tano na sita,ambapo hata matokeo ya mitihani ya Mock mwaka huu yameboreka
Bwalo la chakula lililojengwa Kwa ufadhili Wa GGML katika Shule ya sekondari Bugando wilayani Geita kupitia mradi wa CSR.
Aidha mwl.Gibson ameendelea kusema kuwa, hata wao kama walimu wanajisikia fahari kufanya kazi kwenye mazingira vutivu,huku akieleza kuwa hata wazazi na jamii kwa ujumla imehamasika kwa kuwa hakukuwa na shule ya kidato cha tano na sita kabla, ambapo kwa sasa hawatahangaika tena kutafuta shule mikoa mingine kwa masomo ya A level hasa katika michepuo ya sayansi.
Naye Ibrahimu Maulid Mchana Mwanafunzi wa kidato cha tano shuleni hapo katika mchepuo wa PCB ambaye malengo yake ni kuwa Daktari, amesema kuwa uwepo wa maabara shuleni kwao unawasaidia kufanya tafiti mbalimbali za kisayansi na kupata uzoefu, huku Rebeca Laurent mwanafunzi wa kidato cha nne akisema kuwa uwepo wa wanafunzi wenzao wa kidato cha tano na sita ni faida kubwa kwao, kwa kuwa wanapata wanafunzi wenzao wanaowasaidia katika masomo yao kwa ukaribu zaidi.
Wanafunzi Wa kidato cha nne na tano katika shule ya Sekondari Bugando wakifanya majaribio ya kisayansi katika maabara shuleni kwao iliyofadhiliwa na GGML.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa