Halmashauri ya Wilaya ya Geita imejiwekea mpango wa kukamilisha maboma yote ya miradi ya afya na elimu ifikapo mwezi Disemba 2021.
Mwenyekiti wa Halmashsauri ya Wilaya ya Geita Mh. Charles Kazungu leo Agosti 11, katika kikao cha baraza la madiwani cha kupokea taarifa za utekelezaji wa shuguli za maendeleo katika kila kata kwa mwezi Aprili hadi Juni wamebaini kata nyingi zinakabiliwa na changamoto ya upungufu na ukamilishwaji wa baadhi ya miradi.
Amesema kama Halmashauri wanaendelea kuzifanyia kazi changamoto hizo kuhakikisha wanakamilisha miradi hiyo na kwamba ameagiza kama mwenyekiti wa kamati ya fedha,uongozi na mipango watumishi washirikiane na wataalam wote wa ujenzi wazunguke kata zote ili wabaini maboma ambayo hayajakamilishwa na yanagharama kiasi gani ili yaweze kukamilishwa.
Mheshimiwa Kazungu amesema wanakamilisha maboma ya madarasa hayo mwishoni mwa mwaka huu 2021, ili yaweze kutumika mwakani 2022 kwa wanafunzi watakaoingia kidato cha kwanza.
Baraza la madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Geita limeanza leo Agosti 11, 2021kwa kupokea taarifa kutoka kwa madiwani wa kata zote, ambapo linatarajia kuendelea tena hapo kesho ikiwa ni vikao vya siku mbili mfululizo.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa