Naibu Waziri wa Madini Mheshimiwa Stanslaus Nyong’o amewahakikishia wananchi wa kata ya Nyarugusu kuwa serikali inaendelea kushirikiana nao kuhakikisha wanaishi na kulala salama bila madhara yoyote yatokanayo na athari za migodi hasa milipuko inayosababishwa na wachimbaji wanaomiliki leseni za uchimbaji.
Akiongea na wananchi wa kitongoji cha CCM kuhusu hatma ya malipo waliyokuwa wanalipwa na mgodi wa Pamoja Mine kuwa serikali yao inawalinda na ni kosa la kisheria kwa mmiliki wa mgodi kukubaliana na wananchi kuwalipa malipo hayo ambayo ni kinyume cha sheria bila wizara au tume ya madini kupitia mikataba hiyo.
Mkazi wa kata ya Nyarugusu bibi Pili Bukwimba akitoa malalamiko yake mbele ya Naibu Waziri Nyong'o juu ya usumbufu wanaoupata kutokana na mitetemo inayotoka migodini
Sambamba na hilo Naibu waziri Nyong’o amemuagiza Mkuu wa wilaya ya Geita Mheshimiwa Joseph Maganga kuwachukulia hatua za kisheria wale wote wanaokiuka sheria za uchimbaji wa madini kwa kuwanyanyasa wananchi kwani serikali haitovumilia kuona wananchi wake wananyanyasika.
Aidha katika kuhakikisha haki inatendeka Mkuu wa Wilaya ya Geita ndugu Josephat Maganga amemuagiza kamanda wa Polisi wilaya kuwachukua wamiliki wa leseni hiyo ndugu Mbwana Hassan na Abdallah Kibanda pamoja na Meneja Uendeshaji wa mgodi huo ndugu Hezron Enock ili taratibu za kisheria za kuwafikisha mahakani kwa kukiuka agizo rasmi la serikali la kufunga mgodi huo.
Pichani kushoto ni mmiliki wa leseni ya Uchimbaji bwana Abdallah Kibanda pamoja na Meneja uendeshaji wa Mgodi wa Pamoja Mine bwana Hezron Enock waliokabidhiwa kwa jeshi la Polisi ili taratibu za kisheria ziendelee baada ya kugundulika walikiuka amri halali ya Serikali
Naibu Waziri Nyong’o ameunga mkono agizo la Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel kuufungia mgodi huo kutoendelea na kazi na kuhakikisha wanafuata taratibu zote za kisheria za kuwalipa fidia wananchi wote walioathirika na milipuko hiyo wakati wa uchimbaji.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa