Hamshauri ya Wilaya ya Geita imeibuka mshindi wa jumla wa mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Kwa shule za Msingi Tanzania (Umitashumta) mkoani Geita baada ya kuchukua makombe 10 kati ya 17 pamoja na kombe la Ushindi wa Jumla.
Katibu tawala Mkoa wa Geita Ndugu Mohammed Gombati akikabidhi kombe kwa Mwakilishi wa washindi wa UMITASHUMTA
Mashindano hayo yalijumuisha halmashauri sita za Mkoa wa Geita zilijumuisha wanafunzi zaidi ya 700 kutoka shule za Msingi zote mkoani Geita.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita imeshinda makombe kumi ikiwemo kombe la mpira wa mikono la wasichana, mchezo wa riadha, mpira wa pete (netball) Mchezo wa ngoma, mpira wa miguu Kwa wavulana, mpira wa miguu kwa wasichana, mpira wa wavu kwa wasichana, mpira wa mikono kwa wavulana pamoja na Ushindi wa jumla wa mkoa mzima.
Washindi wa jumla kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Geita wakiwa katika picha ya pamoja na Afisa Elimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Mwl Paul Magubiki kwenye kilele Cha mashindano hayo Mei 29, 2024.
Akizungumzia siri ya kufanya vyema Mwaka huu Ofisa Elimu wa shule za Msingi wa Halmashauri Wilaya ya Geita, Paul Richard amesema ushirikiano, maelewano na umoja baina ya maofisa wa halmashauri na walimu wa shule za msingi ndio chachu ya mafanikio ya halmashauri hiyo kwenye Umitashumita Mwaka huu.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa