Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt Harrison G. Mwakyembe amevisifu na kuvipongeza vikundi vya wajasiariamali vinavyotoka Halmashauri ya wilaya ya Geita kwa ubunifu wa kutengeneza bidhaa tofauti na zenye viwango katika maonesho ya jukwaa la fursa yanaoyoendelea katika viwanja vya GEDECO Halmashauri ya Mji wa Geita.
“Nimeshangaa kuona sofa za kiwango bora kabisa zinatengenezwa na vijana hawa wa Katoro na kuuzwa kwa bei nafuu, nimefurahishwa sana na ubunifu wa kikundi cha walemavu ambao wameamua kuanzisha kiwanda cha kutengeneza viatu,Pia wakina mama watengenezao batiki nao wanafanya vizuri maana malighafi zao wanasema wananunua Tanzania hivyo niwaombe wakazi wa Geita waungeni mkono wajasiriamali hawa maana vitu vyao ni vizuri mno na bei ni rahisi nitatolea mfano hizi sofa,seti moja inauzwa laki tano na nusu wakati ukiipeleka sehemu nyingine inauzwa zaidi ya milioni moja hivyo ni nafuu ya bei karibu mara mbili”. Amesema Mwakyembe
Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo Dkt Harrison G. Mwakyembe akiangalia moja kati ya aina ya viatu vinavyotengenezwa na wajasiriamali kutoka kata ya Katoro wilayani Geita.
Halmashauri ya wilaya ya Geita imekua kimbilio la watu wengi kuangalia na kununua bidhaa mbalimbali kama vile viatu vya ngozi, mafuta ya alizeti,vitambaaa aina ya batiki pamoja na samani za nyumbani ambapo wazalishaji wa bidhaa hizi ni wajasiriamali wa ndani
Maonesho haya yanafanyika katika viwanja vya GEDECO mjini Geita yameratibiwa na ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita kwa kushirikiana na kampuni ya Tanzania Standard Newspaper wachapishaji wa magazeti ya Habari Leo, Daily News na Spoti leo.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa